Uchumi & Biashara
Agricom yatwaa tuzo ya ubora kustawisha kilimo
KILIMO ni biashara kubwa inayopaswa kusimamiwa na kupewa msukuko kutoka sekta mbalimbali. Agricom Africa imeonyesha mfano huo na sasa imezawadiwa.

KAMPUNI ya Tanzania ya Agricom Africa, imetwaa tuzo ya ubora na umahiri kuhudumia na kukuza biashara za kilimo.
Tuzo hiyo ilitoelewa wiki iliyopita katika Jiji la Mumbai, India kutoka kundi la kampuni za Mahindra.
Akipokea tuzo hiyo, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Agricom Africa, Angelina Ngalula, aliishukuru Mahindra kwa kutambua mchango wa kampuni anayoongoza kwa kuthamini mchango wake kwa kuinua wafanyabiashara wanaojihusisha na kilimo.
Angelina alisema kampuni yake imejikita kwenye uwekezaji wa kilimo endelevu na vifaa vya kisasa vinavyokiweka kilimo kuwa njia kuu ya kuondoa umasikini na kukuza ustawi wa Tanzania na nje ya nchi hiyo.