Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Mabadiliko baraza la mawaziri yanukia

Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kutangaza mabadiliko ya baraza lake la mawaziri.

Alhamisi, 27 Agosti 2026 · 18:45Dakika 1 kusoma
Rais Samia akiwa na baadhi ya mawaziri wake katika picha ya kuunganishwa.
Rais Samia akiwa na baadhi ya mawaziri wake katika picha ya kuunganishwa. — Na Maktaba ya Pambazuko

MUDA wowote kuanzia sasa, Rais Samia Suluhu Hassan atafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri, Pambazuko Digital linaweza kueleza.

Taarifa ambazo zimefika chumba cha habari cha gazeti hili jana, zinaeleza kuwa tayari Ikulu inajiandaa kuhabarisha umma kuhusu mabadiliko hayo.

Mabadiliko haya yanafuatia hatua ya Rais Samia kuridhia kujiuzulu kwa makamu wake, Dkt. Emmanuel Nchimbi juzi – Agosti 25 na nafasi yake kujazwa na Deogratius Ndejembi, ambaye alikuwa waziri wa nishati.

Hii ina maana kwamba nafasi ya Ndejembi iko wazi, lakini inaelezwa kuwa Rais Samia, atatumia mwanya huo, kufanya mabadiliko ya mawaziri wake.

“Hapa tunapozungumza Rais Samia ana kikaratasi chake cha majina ya baraza lake analolifanyia tathmini ya mwisho kabla ya kuwapa wasaidizi wake – hasa Katibu Mkuu Kiongozi, ili kuwatangazia Watanzania," amesema mtoa taarifa wetu.

  • samia
  • mawaziri
  • ikulu

Soma Pia