Habari
Mfahamu vyema Deogratius Ndejembi
Jina la Deogratius Ndejembi limepitishwa na vikao vya juu vya CCM kupelekwa bungeni kwa ajili ya kuidhinishwa ili kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya Dkt. Emmanuel Nchimbi kuachia ngazi

DEOGRATIUS Ndejembi, Agosti 26,2026 amepitishwa amepitishwa na vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kupelekwa bungeni kuidhiniwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huo mkubwa, akiwa mtu wa pili kwa ukuu wa nchi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kutamfanya kuanza rasmi wadhifa huo.
Nejembi alipitishwa kwa kauli moja na viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) – ikiwamo kamati kuu ya chama hicho iliyoketi leo, Dar es Salaam.
Ndejembi ametoka wapi?
Waziri huyo wa nishati hadi leo usiku, ni miongoni mwa wanasiasa ambao wamepanda hatua kwa hatua katika uongozi wa serikali na CCM.
Ndejembi alianza kujijenga kisiasa kupitia UVCCM, kabla ya kuingia kwenye nafasi za uongozi wa serikali.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2015, aliteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dodoma, nafasi ambayo aliitumikia kwa miaka kadhaa.
Katika uchaguzi wa mwaka 2020, Ndejembi aligombea na hatimaye kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.
Safari yake ya uongozi iliendelea baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri, akihudumu katika maeneo mbalimbali ya serikali, na baadaye kupandishwa kuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.
Kutoka hapo, Ndejembi aliendelea kupanda kisiasa hadi kufikia nafasi ya waziri wa nishati.
Sasa, jina lake limeibuka tena katika hatua kubwa zaidi baada ya CCM kumpendekeza kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- ndejembi
- nchimbi
- tanzania
- samia
- ikulu