Habari
Mo Dewji achungulia fursa Botswana
BILIONEA wa Tanzania, Mohammed Dewji, ameendelea na safari yake ya "kuchungulia fursa" za kuwekeza na sasa amefika Botswana.

MFANYABIASHARA kutoka Tanzania, Mohammed Dewji, ameendelea kutazama fursa zaidi za uwekezaji Afrika, na sasa “ameweka” mguu Botswana.
Katika kuhakikisha anatumia vyema fursa, Dewji ambaye ni Rais wa Kampuni za MeTL na mtendaji wake mkuu, leo Agosti 26,2026 amekutana na Rais wa Botwana, Duma Boko na kuzungumza.
Rais Boko amemkaribisha Dewji na kuahidi kuunga mkono nia yake kuwekeza Botswana, huku akihimiza “njoo haraka kuchangamkia fursa zilizopo.”
Dewji kwa upande wake amesifu mazingira mazuri na rafiki ya uwekezaji Botswana, huku akisema amepania kuwekeza mtaji mkubwa kwenye viwanda ili kuvuta ajira na ustawi wa wananchi wananchi hiyo tajiri wa madini.
- biashara
- uchumi
- dewji
- boko
- botswana