Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Burudani

Mtoto wa Chameleon matatani Marekani

MTOTO wa mwanamuziki kutoka Uganda, Jose Chameleon, Abba Marcus Mayanja (20), ameripotiwa kukamatwa nchini Marekani na polisi akikabiliwa na tuhuma za shambulio dhidi ya mwanafamilia – lililofanyika nyumbani.

Jumatatu, 17 Agosti 2026 · 17:15Dakika 1 kusomaToleo 178, uk. 38

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na ukurasa wa Facebook wa Minneapolis Safety And Crime Alerts, Abba aliingizwa kwenye kumbukumbu za polisi Agosti 14, 2026, huku picha yake ikiambatana na maelezo ya tuhuma zinazomkabili.

Taarifa hiyo inadai kuwa Abba anachunguzwa kwa kosa la kiwango cha kumfanya mtu mwingine – akiwa ndani ya nyumba, ahofie kupata madhara ya haraka ya kimwili au kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi wakati wa kuchapishwa kwake Abba alikuwa bado anashikiliwa, huku dhamana yake ikitajwa kuwa dola 10,000 za Marekani (zaidi ya Shilingi milioni 27).

Abba Marcus ni mtoto wa kwanza wa Jose Chameleon, amekuwa akiishi na kusoma nchini Marekani.

  • Jose Chameleon
  • Marekani

Soma Pia