Teknolojia
Ndege inayoruka saa 24 angani yaanza safari
Project Sunrise ya Qantas yatimia baada ya miaka kumi ya majaribio; safari ya kilometa 23,075 bila kutua.
Miaka kumi iliyopita, wakati Shirika la Ndege la Qantas la Australia lilipotangaza kuwa limeanza maandalizi ya kuwa na ndege itakayoweza kuruka angani kwa saa 24, ilionekana kama ndoto ya mwendawazimu.
Lakini baada ya maandalizi, majaribio na uwekezaji katika kipindi hicho, mwezi uliopita — Julai — shirika hilo, kwa kushirikiana na kampuni ya kutengeneza ndege ya Airbus, limetimiza azma hiyo na kuifanya ndoto yake isiwe ya mwendawazimu tena.
Ndoto ya shirika hilo ilikuwa ni kuanzisha safari ya moja kwa moja kutoka Australia hadi London, Uingereza, na New York, Marekani. Mradi huo ulipewa jina la Project Sunrise.
Julai 24 mwaka huu, ndege ya shirika hilo aina ya Airbus A350-1000ULR ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Toulouse, Ufaransa, baada ya kuwa angani kwa saa 24 na dakika 24 bila kutua popote, ikitokea moja kwa moja Melbourne, Australia.
Hiyo ni safari ya kilometa 23,075, iliyoweka rekodi na kutimiza ndoto ya Qantas ya kuwa na safari ya moja kwa moja isiyo na kituo.
- Qantas
- Airbus
- Usafiri wa anga
- Teknolojia