Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Ndejembi aula, achukua nafasi ya Dkt Nchimbi

Kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi kumempa 'ulaji' Deogratius Ndejembi.

Alhamisi, 27 Agosti 2026 · 03:47Dakika 1 kusoma
Rais Samia akiwa na Deogratius Ndejembi
Rais Samia akiwa na Deogratius Ndejembi — Na Mpigapicha Wetu

DEOGRATIUS John Ndejembi (43), mjukuu wa mwanasiasa mkongwe nchini, Pancras Ndejembi, ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka mingi, amepitishwa na chama hicho tawala kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Uamuzi huo wa CCM ulipitishwa leo Agosti 26,2026 baada ya halmashauri kuu iliyoketi chini ya mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

Nafasi ya makamu wa rais ilikuwa wazi baada ya aliyekuwa na dhamana hiyo, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuamua kujiuzulu nafasi hiyo jana aliyoitumikia kuanzia Novemba 3, 2025.

Deogratius Ndejembi ambaye ni Waziri wa Nishati, anakuwa Makamu wa Rais wa Tanzania mdogo zaidi kwa miaka ya hivi karibuni.

Nafasi yake inasubiri kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wiki hii ili kuanza kazi rasmi.

  • ndejembi
  • nchimbi
  • tanzania
  • samia
  • ikulu

Soma Pia