Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Ndejembi kuthibitishwa makamu wa rais leo

Baada ya kuteuliwa na vikao vya juu vya CCM, hatimaye leo Bunge linamthibitisha Deogratius Ndejembi kuwa makamu wa rais.

Ijumaa, 28 Agosti 2026 · 07:25Dakika 1 kusoma
Ndejembi
Ndejembi — Kutoka Maktaba ya Pambazuko

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo – Agosi 28, litapokea na kumthibitisha Deogratius Ndejembi kuwa makamu wa rais.

Orodha za shughuli za bunge leo linaloketi jijini Dodoma, zinaonyesha kuwa wabunge watapata fursa ya kumthibitisha makamu huyo mteule kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

Katika historia ya Tanzania haijawahi kutokea uteuzi wa rais ukakumbana na “kigingi” na hata kubalishwa.

Juzi - Agosti 26,2026, Halmashauri Kuu ya CCM ilimpendekeza waziri huyo wa nishati kuwa makamu wa rais.

Ndejembi anachukua nafasi ya Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyetangaza kujiuzulu na baadaye kuvuliwa uanachama na chama chake.

Kwa mujibu wa ratiba ya leo ya Bunge, baada ya wabunge kumthibitisha kazi inayobaki sasa ni kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo tarehe ya shughuli itatangazwa na Ikulu.

  • ndejembi
  • nchimbi
  • tanzania
  • samia
  • ikulu

Soma Pia