Habari
Rais Samia ateua, kuhamisha wakuu wa mikoa
Rais Samia amefanya mabadiliko katika safu ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kadhaa.

RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko katika uongozi wa mikoa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 27,2026 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Abubakar Mussa Kunenge amehamishwa kutoka Pwani na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, akichukua nafasi ya Jabiri Omari Makame ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Beno Moris Malisa amehamishwa kutoka Mbeya kwenda Tabora, akichukua nafasi ya Paul Matiko Chacha, aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni ya CCM.
Adam Malima amehamishwa kutoka Morogoro kwenda Lindi, akichukua nafasi ya Zainab Telack aliyestaafu, huku Queen Cuthbert Sendiga akihamishwa kutoka Manyara kwenda Morogoro.
MAKATIBU TAWALA WA MIKOA
Richard Kayombo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani huku Balandya Mayuganya Elikana akihamishwa Mwanza kwenda Mbeya.
Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga amehamishwa kutoka Singida kwenda Mwanza huku Pili Hassan Mnyema akihamishwa kutoka Pwani kwenda Shinyanga na Rodrick Lazaro Mpogolo kutoka Mbeya kwenda Singida.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa uapisho wa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
- mikoa
- samia
- ikulu