Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Miundombinu

Rais Samia azindua huduma ya mwendokasi Barabara ya Kilwa

Huduma mpya yaanza rasmi katika barabara za Kilwa, Chang’ombe, Sokoine na Kawawa jijini Dar es Salaam.

Jumapili, 9 Agosti 2026 · 11:00Dakika 1 kusomaToleo 177, uk. 3
Rais Samia azindua huduma ya mwendokasi Barabara ya Kilwa
Rais Samia azindua huduma ya mwendokasi Barabara ya Kilwa — Picha na Wizara ya Ujenzi

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekata utepe kuashiria kufungua rasmi huduma ya mabasi ya mwendokasi katika Barabara ya Kilwa, Chang’ombe, Sokoine na Kawawa.

Hafla hiyo ilifanyika Mtoni kwa Aziz Ally, jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Awamu hii inaongeza mtandao wa usafiri wa haraka wa mabasi jijini Dar es Salaam, ambao umekuwa ukipanuliwa kwa awamu tangu kuanzishwa kwake.

  • Mwendokasi
  • Dar es Salaam
  • Miundombinu
  • Rais Samia

Soma Pia