Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Rais Samia: Ndejembi usiende kuwa samaki

Sasa ni rasmi kwamba Deogratius Ndejembi ni Makamu wa Rais wa Tanzania, baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, Dodoma.

Jumamosi, 29 Agosti 2026 · 07:57Dakika 1 kusoma
Deogratius Ndejembi akiapa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania
Deogratius Ndejembi akiapa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania — Na Mpigapicha Wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan amemuasa Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kutumikia taifa kwa utii na kuwa cheo ni dhamana.

Rais Samia ameyasema hayo leo Agosti 29, 2026 wakati wa hafla ya uapisho wa makamu huyo mpya uliofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Usiwe samaki, mheshimiwa Karume mara moja alituasa vijana tusiwe kama samaki kila mkikua akili inaharibika…”

“Kwa hiyo na wewe mwanetu nenda kakue, tumekupa majukumu makubwa, ni imani yangu utaweza,” amesema Rais Samia.

Ndejembi amechukua nafasi ya Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyetangaza kujiuzulu na baadaye kuvuliwa uanachama na chama chake; CCM.

  • ndejembi
  • samia
  • ikulu
  • uapisho

Soma Pia