Haki za Binadamu
Ripoti ya LHRC kuhusu haki yaibua mazito
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu chabaini hatari zinazoongezeka kwa jamii za asili na watetezi wa haki za mazingira.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimebaini uwepo wa athari kubwa za kimazingira ambazo zimetokana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwepo ukame, mafuriko, maporomoko ya ardhi, kuanguka kwa miamba na tope, na ukataji miti.
Ripoti hiyo pia imebaini upungufu wa maji, chakula na malisho kwa maeneo ya jamii za asili, ushindani wa matumizi ya ardhi na rasilimali maji kuongezeka, na uwepo wa migogoro baina ya wakulima, wafugaji na jamii nyingine za asili.
LHRC katika ripoti hiyo imebainisha kuongezeka kwa mazingira ya hatari kwa jamii za asili, na vikwazo katika ushiriki wa kiraia vinavyoathiri kwa kiwango kikubwa zaidi jamii za wachache na jamii za asili.
Ripoti hiyo, ambayo tayari imekabidhiwa serikali na kwa wadau wa mazingira, pia imebainisha kuwa watetezi wa haki za mazingira wanaendelea kukabiliwa na hatari na changamoto mbalimbali wanapotimiza majukumu yao, ikiwepo vitisho, kunyanyaswa, kubughudhiwa kisheria, na vitisho dhidi yao na wanafamilia.
- LHRC
- Haki za binadamu
- Mazingira
- Jamii za asili