Habari Kuu
Shivji aonya kuteka, kutesa binadamu
Vitendo vya watu kutekwa, kuteswa na wengine kupotezwa, vinatajwa kuwa vinadhalilisha utu na hayo yamekemewa pia na Mwanazuoni Profesa Issa Shivji.

MWANASHERIA nguli nchini, Profesa Issa Shivji, amesema matukio ya utekaji, watu kupotea na wengine kuteswa, vinadhalilisha utu wa binadamu.
Profesa Shivji ametoa kauli hiyo leo Agosti 28, 2026, wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa masuala ya demokrasia unaojadili hali ya demokrasia nchini.
Mkutano huo unafanyika katika Makao Makuu ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), jijini Dar es Salaam, ukihusisha wadau mbalimbali wanaojadili masuala ya utawala, haki za binadamu na demokrasia nchini.
Profesa Shivji amesema utu ni msingi muhimu wa maisha ya binadamu na unapaswa kuheshimiwa bila kujali hadhi, cheo au nafasi ya mtu katika jamii.
Amesema vitendo vya utekaji, kupotezwa na kuteswa kwa watu vinakwenda kinyume na misingi ya kuheshimu utu wa binadamu, huku akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinamdhalilisha siyo tu anayetekwa, bali hata mtekaji.
- shivji
- sheria
- tls
- tanzania