Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Wazo Binafsi

Siku ya Vijana Duniani na mustakabali wao Tanzania

KILA ifikapo Agosti 12 kila mwaka, dunia husimama kwa muda kutafakari kuhusu vijana, siyo kwa sababu ni kundi linalohitaji huruma, bali wao ni moja ya nguvu kuu zinazoamua mwelekeo wa dunia ya sasa na ya kesho.

Jumatatu, 24 Agosti 2026 · 06:00Dakika 2 kusomaToleo 179, uk. 22

Mwaka 2026, siku ya vijana duniani iliadhimishwa chini ya kaulimbiu; “mazingira tofauti, matarajio yanayofanana.” Hii inabeba ujumbe mzito.

Kwamba vijana wanaweza kuishi katika mazingira tofauti kabisa, lakini kwa ujumla wanatafuta mambo yanayofanana ambayo ni pamoja na heshima, fursa, usalama, elimu, ajira, uhuru wa kushiriki katika uamuzi na matumaini ya maisha bora.

Umoja wa Mataifa (UN) mwaka huu pia umeweka mkazo katika kuwapa vijana nafasi kubwa zaidi katika uamuzi wa ndani, kitaifa na kimataifa.

Kwa Tanzania, maadhimisho haya yanapaswa kuwa zaidi ya hafla ya kalenda. Yanapaswa kuwa kioo cha taifa; kioo kinachotuonyesha tulipo, tulichofanya kwa vijana wetu, tulichoshindwa kufanya, na muhimu zaidi, aina ya Tanzania tunayowaachia vijana wa leo kuirithi.

Kwa hiyo, swali la msingi katika siku hii ya vijana duniani siyo tumewafanyia nini vijana?” Swali pana zaidi ni; “Je, tumetengeneza Tanzania ambayo kijana anaweza kuishi, kufanya kazi, kubuni, kushiriki na kufanikiwa bila kulazimika kuondoka nchini ili kutafuta mustakabali wake?”

Hili ndilo swali ambalo Tanzania inapaswa kulijibu kwa uaminifu.

Tanzania ni taifa linalobadilika kwa kasi ya kidemografia. Vijana wa miaka kati ya 15 na 35 wanakadiriwa kuunda takribani asilimia 34.5 ya watu wote nchini, jambo linaloifanya Tanzania kuwa na moja ya nguvu kubwa za vijana katika muundo wake wa nguvu kazi.

Takwimu hii haipaswi kusomwa kama namba tu, bali kama taarifa ya kimkakati kuhusu mustakabali wa taifa.

Kwa sababu taifa lenye vijana wengi linaweza kupata kile kinachoitwa faida ya kiuchumi na kijamii inayoweza kutokea pale ambapo sehemu kubwa ya watu iko katika umri wa kufanya kazi, ikiwa taifa lina elimu bora, afya, ajira, ujuzi, uwekezaji na taasisi zinazowezesha uzalishaji.

Lakini mgawanyo wa kiuchumi, si zawadi inayokuja yenyewe, ni fursa inayohitaji maandalizi. Ikiwa vijana wana elimu lakini hawana ajira, mgawanyo wa kiuchumi inaweza kugeuka kuwa manufaa yatokanayo na hali ya kukatishwa tamaa.

Ikiwa wana nguvu lakini hawana fursa, nguvu hiyo inaweza kugeuka kuwa kukata tamaa.

Ikiwa wana mawazo lakini hawana mazingira ya kuyatekeleza, ubunifu unaweza kuhamia nchi nyingine.

  • Vijana
  • Demokrasia

Soma Pia