Habari Kuu
Taharuki Taarifa za Nchimbi Kujiuzulu
TAARIFA za Makamu wa Rais, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kujiuzulu nafasi yake zimetikisa mitandao ya kijamii nchini Tanzania.

Kwa takribani dakika 30 hivi, kuanzia leo saa 5 asubuhi - Agosti 25, 2026; mitandao ya kijamii imeenea au kusomeka barua inayodaiwa imeandikwa na Dkt. Nchimbi ambapo ameeleza kuwa tayari amemjulisha Rais Samia Suluhu Hassan juu ya hatua hiyo.
Ingawa hakueleza kwa undani sababu za kuchukua hatua hiyo ngumu ambayo hazijawahi kutokea katika awamu zote zilizopita, Dkt. Nchimbi ameeleza kwa kifupi kuwa anaamini Rais Samia anataka mabadiliko.
Pamoja na taarifa hiyo kusambaa kutoka akaunti binafsi ya Dkt. Nchimbi, mitandao rasmi ya serikali, ikiwamo ya Ikulu haijatangaza lolote.