Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Uchumi & Biashara

Tanzania yalenga kunufaika zaidi na soko la hewa ukaa

Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni chapewa jukumu la kuvutia uwekezaji wa kijani na kuimarisha mifumo ya usimamizi.

Jumatatu, 10 Agosti 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 177, uk. 18

Wakati dunia ikiweka mkazo kwenye biashara ya hewa ukaa, Tanzania nayo imeamua isiachwe nyuma katika safari hiyo.

Sasa Tanzania imetangaza mipango kadhaa inayolenga kuiwezesha nchi kupata sehemu kubwa zaidi ya mapato kupitia soko la hewa ukaa linalokua kwa kasi duniani.

Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kimepewa jukumu la kuimarisha mifumo ya usimamizi, kuvutia uwekezaji wa kijani, na kuongeza manufaa yatokanayo na rasilimali asilia za nchi.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Muyungi, amesema Tanzania inapaswa kubadilika kutoka kuwa mshiriki wa kawaida katika soko la hewa ya ukaa na kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kujenga mifumo thabiti inayowezesha utekelezaji wa miradi yenye viwango vya juu vya uadilifu wa kaboni.

Akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya Wakurugenzi ya NCMC kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kilichofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Dkt. Muyungi alisema uchumi kupitia hewa ya ukaa ni fursa muhimu kwa taifa.

  • Hewa ukaa
  • NCMC
  • Mazingira
  • Uwekezaji

Soma Pia