Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Tume ya Uchunguzi

Wadau waingiwa hofu uhalali wa Tume ya Jinai

Upingaji wa tume iliyozinduliwa na Rais Samia umevuka mipaka, ukiibuka hata Namibia anakotoka mmoja wa wajumbe wake.

Jumatatu, 10 Agosti 2026 · 04:30Dakika 1 kusomaToleo 177, uk. 20
Tume ya Uchunguzi
Tume ya Uchunguzi — Picha na Mwandishi Wetu

Hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua Tume ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai yenye jukumu la kuchunguza vurugu zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imewaibua wadau mbalimbali wakipinga uhalali wake.

Tume hiyo haipingwi tu hapa nyumbani, kwani hata huko Namibia, ambako anatoka mmoja wa wajumbe wake, kumeibuka upingaji pia.

Taasisi inayojihusisha na harakati za kisiasa nchini Namibia, Affirmative Repositioning (AR), imepinga uteuzi wa Jaji Mkuu Msaidizi wa Namibia, Petrus Tileinge Damaseb, kushiriki kwenye tume hiyo.

Tume hiyo yenye wajumbe sita — wanne kutoka Tanzania na wengine wawili wakitoka nje ya Tanzania, mmoja kutoka Uganda na mwingine Namibia — ilizinduliwa na Rais Samia, Agosti 7, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Tume hiyo mpya inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shabani Lila, ni sehemu ya utekelezaji wa hatua zilizopendekezwa baada ya kuundwa kwa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Matukio ya Vurugu za Oktoba mwaka jana.

  • Rais Samia
  • Tume ya Uchunguzi
  • Uchaguzi Mkuu

Soma Pia