Kila wakati unapojiandikisha kupokea nakala ya bure ya gazeti la Pambazuko, tunahakikisha usiri na usalama wa mawasiliano yako uko katika ulinzi wa hali ya juu.
Nambari ya simu na anwani ya barua-pepe ya kila msomaji wetu, ni salama kabisa, kwani hatuna kikundi cha kuwaweka wale wanaojiunga pamoja. Kila mmoja hutumiwa binafsi na siyo kwenye makundi.
Gazeti la kidijitali la Pambazuko ni la bure kwa kila mtu na linawahimiza wasomaji wote kulisambaza kwa wengine bila ubaguzi, hata kwa wale ambao hawaelewi Kiswahili, ili wapate nguvu ya kujifunza.
Uongozi wa Pambazuko unaamini kuwa ni haki kwa kila binadamu kupata habari na taarifa bure – kama ilivyo kwa hewa.
Ni matamanio yetu kuwa gazeti la Pambazuko liendelee kusambazwa bila malipo wakati wote, japo tunawahimiza wasomaji wetu watuunge mkono kwa kututumia kiasi chochote cha fedha wanachoweza, ili tuendelee na uandishi bora wa habari.
Ni michango ya rasilimali fedha kutoka kwa wasomaji wetu na watu wengine, hasa wanaoamini katika uandishi bora wa habari, ndiyo itakayohakikisha uwepo wetu na kuboresha zaidi kazi zetu.
Unaweza kutuchangia kupitia nambari ya simu ya Mpesa – 0744 768 263. Pia tunapokea michango ya benki ambayo inaweza kutumwa kwetu kupitia akaunti ifuatayo:
- Jina la Benki: Tanzania Commercial Bank
Jina la Akaunti: Tanzania Media Practitioners AssociationNamba ya Akaunti: 111218000602
Swift Code: TAPBTZTZ
Tunakubali kiasi chochote cha pesa; kikubwa ama kidogo, kwetu ni shukrani.
Pambazuko ni gazeti la watu. Ni gazeti la kila mtu, halimbagui mtu yeyote kwa misingi ya itikadi za kisiasa, kidini, kifalsafa au kiuchumi.
Kwa msingi huo, ni gazeti lisilo na mrengo wowote wa kisiasa. Ni jukwaa huru la kuongeza ufahamu, maarifa na uwazi kwa lengo la kusaidia kuwafikia watoa uamuzi kutenda haki na kujali wananchi.
Kila mtu anaruhusiwa kuandika makala, maoni, barua na hata habari, ambazo zitapitiwa na kuhaririwa na wahariri wetu ili kuboresha na kuendana na sera ya uhariri ya Pambazuko.
Mpaka sasa Pambazuko halina mpango wa kuchapishwa katika karatasi. Litaendelea kusambazwa bila malipo katika mfumo wake wa kidijitali kupitia jukwaa la WhatsApp na mitandao mingine ya kijamii. Hata hivyo, endapo kutajitokeza fursa, tuko tayari kulichapisha kwa masharti ya kuendelea kuwa bure.
Matoleo yote yaliyopita ya Pambazuko yanapatikana kwenye tovuti ya gazeti hili hapa: www.pambazuko.or.tz
Ndio, tunapokea na kuchapisha matangazo kwa gharama nafuu zaidi. Matangazo pia ni njia nyingine ya kuchangia uhai wa gazeti la Pambazuko. Hata hivyo, hatupokei kila tangazo, sera yetu ya uhariri, inazuia kupaisha matangazo ya wauza unga, wauza silaha na biashara ya ngono.
Ndiyo, Pambazuko linatarajia kuwa na baadhi ya kurasa chache zilizochapishwa kwa Kiingereza na pia lugha zingine za kienyeji za Kiafrika, endapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.
Ndiyo, mawasiliano rasmi ya Pambazuko ni haya yafuatayo:Simu: +255 744 768 263 na pia barua pepe: info@pambazuko.or.tz