Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Kuhusu Sisi

Pambazuko ni neno la Kiswahili ambalo tafsiri yake nyingine ni mawio; kuanza kwa jambo au siku.

Hili ni jina la gazeti la watu wa kada zote; gazeti la ubunifu la kila wiki, linaloandikwa kwa lugha ya Kiswahili — lugha inayounganisha zaidi ya wazungumzaji milioni 300 duniani kote.

Gazeti hili limeanzishwa kwa msukumo wa kuhakikisha kuwa kila mtu anapata habari kwa gharama nafuu. Tunaamini katika haki ya kupata habari, na ndiyo maana Pambazuko limekuwa likitolewa bure tangu kuanzishwa kwake.

Pambazuko ni gazeti linalosambazwa kupitia WhatsApp na pia kwa njia zingine za kimtandao; Signal na barua pepe. Msomaji anaweza pia kusoma matoleo yetu kupitia tovuti hii.

Dhamira Yetu

Lengo letu ni kuwawezesha waandishi kufanya kazi zao kwa uhuru, kuwapa wananchi nguvu kupitia vyombo bora vya habari, na kujenga madaraja yanayounganisha wasomi, watunga sera na wananchi — bila kujali kiwango cha elimu, kipato au imani zao.

Ahadi Yetu Kwa Msomaji

  • Hatutachapisha habari ambayo hatuwezi kuisimamia.

  • Tutajirekebisha hadharani pale tunapokosea.

  • Tutawalinda vyanzo vyetu wanaohatarisha usalama wao kuzungumza nasi.

  • Hatutaruhusu matangazo au ushirikiano wa kibiashara kuathiri maamuzi yetu ya kiuhariri.

Mhariri Mkuu

Simon Mkina — Mwanzilishi na Mhariri Mkuu. Mwandishi wa habari za uchunguzi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 33. Aliwahi kuwa mhariri wa magazeti mengi ya ndani na nje ya Tanzania. Ni mshirika wa muda mrefu mashirika na taasisi kubwa za habari za kimataifa, ikiwamo ICIJ. Hivi sasa ni Rais wa Chama cha Wanahabari Tanzania (Tampa).