Maswali
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara na wasomaji wetu.
Je, mawasiliano yangu ni salama kiasi gani ninapojisajili?
Kila wakati unapojiandikisha kupokea nakala ya bure ya gazeti la Pambazuko, tunahakikisha usiri na usalama wa mawasiliano yako uko katika ulinzi wa hali ya juu.
Namba za simu na anwani za barua pepe za wasomaji wetu zinabaki salama, na hazitolewi wala kuuzwa kwa mtu au taasisi yoyote.
Kwa nini Pambazuko linasambazwa bure?
Gazeti la kidijitali la Pambazuko limekuwa likitolewa bure kwa kila mtu tangu kuanzishwa kwake, kwa sababu uongozi wetu unaamini ni haki ya kila binadamu kupata habari.
Pambazuko inahusishwa na itikadi gani?
Pambazuko ni gazeti la watu, lisilo na mrengo wowote wa kisiasa. Wote wanaruhusiwa kuchangia mawazo yao, bila kujali itikadi zao.
Ninawezaje kuchangia?
Unaweza kuchangia kupitia M-Pesa namba 0744 768 263, au kupitia Tanzania Commercial Bank (TCB) akaunti namba 111218000602.
Pambazuko litapatikana lini kwa nakala ngumu (hard copy)?
Kwa sasa hakuna mpango wa kuchapisha gazeti karatasini. Pambazuko litaendelea kusambazwa kwa njia ya kidijitali.
Je, Pambazuko linapokea matangazo ya kulipia?
Ndiyo, tunapokea matangazo. Lakini hatupokei kila tangazo — kila tangazo hupimwa kulingana na sera yetu ya uhariri.
Hatupokei matangazo ya kamari, sarafu za kidijitali zisizodhibitiwa, wala matangazo ya vyama vya siasa katika kipindi cha uchaguzi.
Nitapata gazeti la Pambazuko bure hadi lini?
Toleo la wiki linaloenda kwa WhatsApp, Signal na barua pepe litaendelea kuwa bure.
Kwenye tovuti, habari za dharura na za maslahi ya umma zitaendelea kuwa wazi kwa kila mtu. Kila msomaji pia anapata makala matatu bure kila mwezi.
Rasimu — inasubiri idhini ya mhariri mkuu.
Kwa nini sasa mnaanzisha uanachama wa kulipia?
Habari za uchunguzi zinagharimu muda, safari, ulinzi wa vyanzo na wakati wa mawakili. Uanachama unatuwezesha kulipa gharama hizo bila kutegemea mtu mmoja au taasisi moja.
Msomaji asiyeweza kulipa hataachwa nyuma: toleo la WhatsApp linabaki bure, na habari muhimu za umma zitabaki wazi.
Rasimu — inasubiri idhini ya mhariri mkuu.
Ninawezaje kulipia uanachama?
Utaweza kulipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au kadi ya benki.
Mfumo wa malipo bado unaandaliwa na utatangazwa pindi utakapokamilika.
Rasimu — inasubiri idhini ya mhariri mkuu.