Habari
Laini moja ya simu kutumika nchi 190
WASAFIRI wanaokwenda nje ya Tanzania, sasa wataweza kupata huduma ya intaneti bila kubadilisha laini zao za simu au kununua kadi za simu wanapowasili, baada ya kuzinduliwa kwa jukwaa la Kwetu eSIM.

Huduma hiyo inayopatikana katika nchi 190 duniani inawawezesha watumiaji kununua vifurushi vya intaneti kabla ya kuanza safari na kuviwasha wanapowasili katika nchi wanayokwenda kupitia simu zinazotumia teknolojia ya eSIM.
Kwa majibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa iliyotolewa na Kampuni ya Kwetu eSIM, kupitia programu hiyo, mtumiaji anaweza kuchagua nchi anayokwenda, kununua kifurushi cha data na kukiwezesha kwa kutumia QR code au msimbo wa kuwezesha huduma hiyo, bila kulazimika kutoa Sim kadi iliyopo kwenye simu.
Imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kupunguza changamoto ambazo wasafiri hukutana nazo wanapokuwa nje ya nchi, ikiwamo gharama kubwa za huduma za roaming, usumbufu wa kutafuta kadi za simu simu za nchi husika na kulazimika kusubiri katika maduka ya huduma za mawasiliano baada ya kuwasili.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kuwa Kwetu eSIM pia inaruhusu malipo kwa kutumia kadi pamoja na huduma za fedha kwa mitandao yote ya simu huku maelezo yote yakiwa yanaoatikana kupitia tovuti ya kwetuesim.com au https://kwetuesim.com/sw/.
Imeeleza kuwa watumiaji pia wanaweza kuweka fedha kwenye pochi ya ndani ya programu hiyo kwa ajili ya kufanya malipo.
Huduma hiyo imeelezewa kuwa inaweza kutumiwa na wasafiri wa kibiashara, watalii, wanafunzi, watu wanaokwenda kutembelea familia nje ya nchi pamoja na kampuni zinazowapeleka wafanyakazi katika safari za kimataifa.
Miongoni mwa huduma zinazopatikana ni uwezo wa kuongeza kifurushi cha data mtumiaji anapokaribia kukimaliza akiwa nje ya nchi. Mtumiaji hahitaji kuondoa au kusakinisha upya eSIM yake ili kuongeza data.
Pia, mtumiaji anaweza kumnunulia mtu mwingine kifurushi kama zawadi. Kipengele hicho kinaweza kutumiwa na mtu anayemtayarishia ndugu, rafiki au mfanyakazi wake huduma ya mawasiliano kabla ya kusafiri.
Kwa mujibu wa maelezo katika taarifa yao, huduma hiyo inapatikana katika zaidi ya nchi 190 na inahudumia maeneo ya Afrika, Ulaya, Asia-Pacific, Amerika na Mashariki ya Kati.
Programu hiyo inapatikana katika mifumo ya iOS, Android na Huawei, huku ikisaidia lugha saba ambazo ni kiingereza, kiswahili, kifaransa, kihispania, kiitaliano, kiarabu na kichina.
Huduma hiyo pia inaonyesha matumizi ya data kupitia vipengele vinavyopatikana kwenye skrini ya simu, hatua inayomwezesha mtumiaji kufuatilia matumizi yake na kuongeza kifurushi anapohitaji.
“Uzinduzi wa Kwetu eSIM unakuja wakati matumizi ya simu janja na huduma za kidijitali yakiendelea kuongezeka, huku wasafiri wakihitaji njia rahisi ya kuendelea kutumia intaneti bila kutegemea huduma za roaming za waendeshaji wa simu wa nchi wanayotoka.
Kwetu eSIM imesema watumiaji wanaweza kupata huduma hiyo kupitia Apple App Store na Google Play, huku vifurushi pia vikipatikana kupitia tovuti ya kampuni.
Kampuni hiyo imeeleza kuwa lengo lake ni kuunganisha huduma za mawasiliano za kimataifa na njia za malipo zinazopatikana katika masoko ya ndani, ili kurahisisha upatikanaji wa intaneti kwa wasafiri.
Hata hivyo, upatikanaji na matumizi ya eSIM hutegemea kama simu ya mtumiaji inaunga mkono teknolojia hiyo pamoja na masharti ya mtandao katika nchi anayokwenda.
- eSIM
- Teknolojia
- Mawasiliano
- Safari