Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Uchumi & Biashara

Viwanda vya baruti vyaingia msasa

Msasa imeingia kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa muhimu katika sekta ya madini.

Jumatatu, 24 Agosti 2026 · 06:00Dakika 2 kusomaToleo 179, uk. 18

Pwani sasa imeingia katika uzalishaji wa baruti na vilipuzi, bidhaa ambazo hutumika kwenye shughuli za uchimbaji madini, lakini hazizalishwi kwa wingi nchini.

Taarifa iliyotolewa wiki iliyopita inaeleza kuwa viwanda viwili vya baruti na vilipuzi vinajengwa katika wilaya ya Kisarawe mkoani humo.

Ujenzi wake utakapokamilika viwanda hivyo vitaongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa bidhaa hizo ndani ya nchi na kupunguza uagizaji wake nje ya nchi.

Viwanda hivyo vimetajwa kuwa ni Ideal Detonators Tanzania Limited, kinachotarajiwa kuwa miongoni mwa viwanda vikubwa vya aina hiyo Aidha, kwa upande wa vilipuzi, alisema mahitaji yapo kwenye vipande 29,663.17 kwa mwaka hivyo uwekezaji huo ni muhimu kwa kuwa utaongeza uzalishaji wa ndani wa bidhaa hizo.

Dkt. Kiruswa alisema uwekezaji huo unaonesha utekelezaji wa dhana ya uongezaji thamani madini, kwa kuwa Tanzania inalenga siyo tu kuchimba madini, bali pia kuzalisha bidhaa kutokana na madini hayo yanayochimbwa nchini.

“Baruti ni miongoni mwa bidhaa muhimu katika shughuli za uchimbaji madini, kwani huwezesha wachimbaji kuyafikia madini…”

“Uzalishaji wa bidhaa hizi hapa nchini utaongeza upatikanaji wake na kupunguza utegemezi wa uagizaji bidhaa kutoka nje,” alisema Dkt. Kiruswa.

Kuhusu changamoto ya soko la ndani iliyowasilishwa na Solar Intracom Chemicals, Dkt. Kiruswa alisema wizara inalichukua suala hilo kwa uzito na italishughulikia kwa kushirikiana na wadau, ili kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinapata soko na viwanda vinaendelea kuzalisha.

Alisema ikiwa serikali imeweza kushughulikia changamoto zilizowahi kujitokeza katika sekta nyingine za uzalishaji ikiwemo chumvi, hivyo ina imani kuwa changamoto zinazokabili uzalishaji wa baruti na vilipuzi nazo zitapatiwa ufumbuzi.

Udhibiti Uzalishaji wa vilipuzi nchini siyo shughuli ya kawaida ya viwanda. Chini ya sheria ya vilipuzi sura ya 45, mtu haruhusiwi kutengeneza vilipuzi bila kuwa na leseni au kibali halali.

Sheria pia inadhibiti uagizaji, usafirishaji, uuzaji, umiliki, uhifadhi na matumizi ya vilipuzi.

Aidha, kanuni za sheria hii za mwaka 2019 zinaweka masharti maalumu kwa viwanda vya vilipuzi, yakiwemo mahitaji ya kupata idhini kabla ya ujenzi, hatua za usalama, ulinzi wa malighafi na bidhaa, mafunzo ya Watanzania, utunzaji wa kumbukumbu na utoaji wa taarifa za uzalishaji kila mwezi.

Tume ya Madini pia inaeleza kuwa mwombaji wa leseni ya kutengeneza vilipuzi anatakiwa kuwasilisha michoro na mpangilio wa kiwanda, barua kutoka kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, kufanyiwa ukaguzi na Tume ya Madini kabla na baada ya ujenzi, pamoja na kupata maoni ya Firearms and Ammunition Control National Committee.

Kwa mtazamo wa biashara Hili ni eneo lenye fursa kubwa lakini lenye vizingiti vikubwa vya kuingia. Mahitaji yake yanaendeshwa zaidi na ukuaji wa sekta ya madini, ujenzi wa miundombinu na uchimbaji wa mawe.

Kwa Tanzania inayolenga kuongeza uzalishaji wa madini na kuongeza thamani ndani ya nchi, uzalishaji wa vilipuzi ni sehemu muhimu ya kukuza uzalishaji wa ndani katika mnyororo wa thamani wa madini.

  • Viwanda
  • Madini

Soma Pia