Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari

Wafanyakazi IPTL waiangukia serikali iwalipe

BAADHI ya waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), wameiomba serikali iharakishe malipo ya stahiki zao ili waweze kutafuta makazi mapya.

Jumatatu, 7 Septemba 2026 · 06:00Dakika 2 kusomaToleo 181, uk. 15

Wafanyakazi hao wameomba hivyo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, kubariki kuondolewa kwao kwenye nyumba za kampuni hiyo.

Wameliambia Gazeti la Pambazuko kuwa kwa sasa hawana mahali pa kuishi wao na familia zao wakiwamo watoto, hivyo wanaiomba serikali kupitia Hazina iharakishe kuwalipa stahiki zao ambazo wanaidai kampuni hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya serikali baada ya mgogoro uliokuwepo kati yake na mmiliki, Harbinder Sing Sethi, kuamuliwa na Mahakama Kuu.

Wafanyakazi hao ni waliokuwa wameombwa na uongozi wa kampuni ya IPTL kulinda mitambo, magari pamoja na nyumba kadhaa zilizokuwa makazi ya maofisa wa kiwanda na walipewa mikataba ya kuendelea kuishi hapo hadi watakapokuwa wamelipwa stahiki zao Hazina.

Mmoja wa wafanyakazi hao, Willbroad William, amesema wameshangazwa na kauli ya mkuu huyo wa wilaya, Mtambule, kuwaamuru waondoke bila kujali kuwa wako na familia, lakini kikubwa bado wanaidai serikali stahiki zao.

Wafanyakazi hao wamesema baada ya kampuni hiyo kufungwa, waliokuwa wakurugenzi; Ambroce Brixson Lugenge kwa niaba ya mwenyekiti (Seth) na Joseph Makandege (mwanasheria) waliwakabidhi nyumba hizo na mali zingine kwa mkataba maalum kwamba waendelee kuzilinda wakati wanasubiri malipo yao.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake, mfanyakazi mwingine amesema baada ya Vifaa vya ndani vikiwa vimetupwa nje ya nyumba za IPTL zilizoko Salasala, Dar es Salaam kama vilivyokutwa juzi.

kiwanda cha IPTL kufungwa na serikali na baadaye aliyekuwa mmiliki wake, Sethi, kuwekwa rumande, waliokuwa wakurugenzi wa kampuni hiyo waliwapa barua za kuwaondoa kazini zikiambatana na madai na stahiki za kila mfanyakazi.

“Leo (Jumamosi Septemba 5, 2026) Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amekuja hapa na kuamuru tuondoke, akisema hizi nyumba ni mali ya Sethi, kwa kuwa sisi hatuna cha kufanya, tunaomba serikali kupitia Hazina watulipe mafao yetu…”

“Hapa tunapoongea tumefungiwa nje ya geti, haturuhusiwi kuonekana kwenye eneo hili, tunaamini Rais Samia Suluhu Hassan asingependa kuona tunanyanyasika kiasi hiki, tunamuomba asikie kilio chetu, watulipe ili tutafute mahali pa kujistiri na familia zetu, hata fedha za kuhamisha mizigo yetu hatuna,” amesema mmoja wa wafanyakazi hao Akaongeza; “Kwa sasa tupo tunahangaika kuhamisha familia zetu, hatujui hata tunaelekea wapi, tangu awali sisi hatukuwa wakaidi kuondoka kwenye hizi nyumba, bali tulikuwepo kwa sababu hatujalipwa fedha zetu ambazo tunadai kwa mujibu wa sheria.”

Akizungumza na wafanyakazi hao, Jumamosi Septemba 5, 2026 Mtambule aliwataka wafanyakazi hao ambao alidai kuwa ni walinzi waliokuwa wanaishi katika nyumba za IPTL zipatazo 12 kuondoka mara moja.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • IPTL
  • Wafanyakazi
  • Nishati

Soma Pia