Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Dunia yatega masikio leo hukumu ya Lissu

Kiongozi wa upinzania Tanzania, Tundu Lissu na dunia, "wako macho" kufuatilia hukumu ya mwenyekiti huyo wa Chadema. Kuna mawili; kuachwa huru ama kuhukumiwa kifo au vinginevyo.

Ijumaa, 6 Novemba 2026 · 08:00Dakika 1 kusoma
Lissu
Lissu — Picha kutoka Maktaba ya Pambazuko

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo; Ijumaa, Novemba 6, 2026, asubuhi inatoa hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.

Ulinzi umeimarishwa katika eneo la mahakama, ambako jopo la majaji watatu linatarajiwa kusoma uamuzi huo.

Jaji Dunstan Ndunguru anaongoza jopo hilo, akishirikiana na majaji; James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Mahakama ilipanga tarehe ya hukumu baada ya upande wa mashtaka na utetezi kuwasilisha hoja zao za mwisho Septemba 29

Lissu anakabiliwa na shtaka chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Upande wa mashtaka unadai kuwa Aprili 3, 2025, alitoa kauli zilizolenga kuhamasisha wananchi kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo kwa nia ya kuitishia Serikali.

Mwenyekiti huyo wa chaama cha upinzani, alikamatwa Aprili 9, 2025, baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Mbinga, mkoani Ruvuma, na alifikishwa mahakamani siku iliyofuata.

Jopo hilo litaamua iwapo upande wa mashtaka umethibitisha shtaka dhidi ya Lissu. Iwapo atapatikana na hatia, suala la adhabu litafuata. Katika hoja za mwisho, Lissu alieleza kuwa kifungu hicho kinaweka adhabu ya lazima ya kifo kwa kunyongwa au kuachiwa huru endapo itamuona hana hatia.

Hata hivyo, wakili wa mkuu wa serikali, Nassoro Katuga, alitoa tafsiri tofauti, akisema mahakama ina mamlaka ya kutoa adhabu ya kifungo badala ya kifo, kadri itakavyoona inafaa.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • Lissu
  • Hukumu
  • Kifo
  • Uhaini
  • Mahakama

Soma Pia