Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Mitindo & Urembo

Fascinator: Pambo la kichwani linalobamba

FASCINATOR ni miongoni mwa vifaa vya urembo vinavyoweza kuongeza mvuto wa pekee katika muonekano wa mwanamke.

Jumatatu, 14 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 182, uk. 35

Tofauti na kofia za kawaida, kazi ya kuu fascinator ni kurembesha na kuongeza nakshi kwenye vazi lako.

Ili uonekane wa kisasa ni muhimu uzingatie mpangilio wake kulingana na aina ya vazi, rangi na mtindo wa nywele.

Fascinator inaweza kuwekwa upande mmoja wa kichwa, mbele kidogo au juu kulingana na umbo la uso na muundo wake.

Kwa mavazi yenye rangi tulivu, fascinator yenye rangi au mapambo yanayovutia inaweza kuongeza mvuto.

Pia fascinator yenye mapambo mengi inapaswa kuvaliwa na mavazi yasiyo na mapambo mengi ili kuepuka mwonekano uliozidi.

Kwa hafla kama harusi au sherehe yoyote, fascinator inaweza kuambatana na gauni, suti au vazi la ‘two-piece’.

  • Mitindo
  • Urembo

Soma Pia