Mitindo & Urembo
Prisca Lyimo katika vazi la kipekee usiku wa Miss Cosmo
MWANAMITINDO na muigizaji, Prisca Lyimo, amevikwa rasmi taji la Miss Cosmo Tanzania 2026 kwenye usiku wa fainali kuu ya mashindano ya Miss Grand Tanzania na Miss Cosmo Tanzania.

Kama mshindi wa taji hilo, Prisca anajiandaa kuiwakilisha Tanzania kimataifa nchini Vietnam.
Muonekano wake uliyoandaliwa na chapa ya hapa nyumbani ya Neste Fashions, uliuteka uwanja na kuvutia macho ya watazamaji.
Gauni lake la kipekee limebuniwa na chapa mashuhuri ya mavazi nchini ya Neste Fashions.
Pia vazi lake hilo limetawaliwa na mchanganyiko wa rangi za kifahari za royal blue na purple zilizopambwa kwa ufundi wa juu wa mawe na shanga zinazong’aa.
Gauni hilo likiwa na mikono mirefu ya kitambaa chepesi huku shingo ikiwa ya wazi iliyoshuka chini na mpasuo mrefu unaoleta muonekano wa kisasa.
Mrembo huyo amenogesha muonekano wake na viatu virefu vya wazi pamoja na mtindo wa nywele fupi zilizowekwa vizuri upande mmoja.
Fanya ngozi ya uso kuwa laini
NGOZI ya usoni inavutia kutokana na matunzo haswa kwa kufuata ratiba bora kuanzia namna ya kuosha hadi vitu unavyovitumia.
Hapa nimekuwekea vitu vingine vya kubusti mwonekano wako kama ifuatavyo; Tumia mafuta ya vaseline ya mgando kijiko kimoja na kiini cha yai.
Osha vizuri uso wako kisha kausha vizuri.
Changanya mafuta na kiini cha yai koroga vyema na upake usoni kwa kujimasage, kaa na mchanganyiko usoni kwa dakika 30, kisha nawa kwa maji safi ya uvuguvugu usitumie sabuni.
Fanya hivi mara mbili kwa wiki na utaona matokeo.
- Mitindo
- Urembo
- Miss Cosmo