Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Michezo

Jeshi Stars, Magereza, mabingwa TVNL

KLABU ya wanaume ya mpira wa wavu, Jeshi Stars, imetwaa ubingwa wa Ligi ya Taifa Mpira wa Wavu Tanzania TVNL 2026, huku Magereza kwa wanawake waking’ara kwa mara ya sita mtawalia.

Jumatatu, 21 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 183, uk. 37

Jeshi Stars ilitwaa ubingwa huo usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita kwa kuichakaza Bandari kwa seti 3-1 za (25-23), (25-23), (17-25) na (25-22) katika fainali zilizolindima kwenye Uwanja wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania ‘TVF Arena’ uliopo Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam.

Haukuwa mchezo rahisi kwa Jeshi Stars licha ya kuibuka mabingwa, kutokana na upinzani ambao Bandari waliuonyoshe katika seti zote huku wakipoteza kwa kukosa umakini wa kulinda uongozi wao ambapo walikuwa wamefanikiwa kuongoza seti zote nne.

Huo ni ubingwa wa pili kwa makamanda, ambapo mara ya kwanza walitwaa ubingwa huo msimu wa 2022, fainali zilizopigwa uwanja wa ndani wa Taifa, huku kwa upande huo wa wanaume, Tanzania Prisons, High Voltage, KIUT na JKT zimewahi kutwaa ubingwa huo.

Kwa upande wa ligi ya wanawake, mabingwa mara nyingi zaidi klabu ya Magereza waliibuka mabingwa kwa kuichalaza Bandari kwa seti 3-2.

Ulikuwa mcheo mgumu kwa pande zote mbili kutokana na upinzani ambao Bandari waliutoa katika seti zote tano kwa mabingwa hao wa TVNL, ikiwa ndio klabu yenye mafanikio makubwa kwenye ligi ya wanawake.

Msimu wa sita wa TVNL, Tanzania Prisons (W) wamewaweka wapinzania wao nyuma ya nondo bila kujali ubora ambao wamekuwa wakiuleta katika kila msimu na kushindwa kufuadafu.

Kongole kwa Jeshi Stars kutwaa ubingwa wa pili kwa kuwavua mabingwa watetezi Chuo Kikuu cha Kampala (KIUT) na Magereza kuendeleza moto na utawala wa TVNL.

Msimu huu umekuwa wa mafanikio makubwa kwa TVF kwa namna ambavyo wameendesha ligi kwa viwango vya kimataifa, miundombinu bora na ongezeko la wadhamini ambao wameongeza chachu katika Ligi ya Taifa ya Wavu 2026.

  • Mpira wa Wavu
  • TVNL
  • Jeshi Stars
  • Magereza
  • Michezo

Soma Pia