Michezo
Utamu warejea Mwembeyanga
BAADA ya mapunziko ya wiki kadhaa, hatimaye utamu wa Ligi Kuu Mchezo wa Wavu Tanzania (TVNL 2026) umerejea Septemba, 06, 2026 katika Uwanja wa TVF uliopo Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salama kwa miamba ya klabu 24 kumenyana mzunguko wa pili.
Ligi hiyo, inayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) ilianza mzunguko wa kwanza mwanzoni mwa Agosti na kushuhudiwa upianzani mkubwa kwa klabu 14 za wanaume na 10 za wanawake.
Katika michezo aaba ya mzunguko wa kwanza kwa upande wa wanaume, Bandari VC walipata ushindi na kuongoza msimamo kwa pointi 20 pasipo kupoteza mchezo wowote. Nafasi ya pili ilishikiliwa na High Voltage kwa pointi 18, wakishinda sita na kupoteza mmoja.
Hali itakuwaje kwenye mzunguko wa pili kuelekea mzunguko wa tatu hadi fainali? Kinachozungumzwa hapa ni ufundi na vita ya kushinda michezo na seti zilizoko mbele yao.
Timu za Jeshi Stars, Nyika pamoja na JKT bado wanaweza kupindua msimamo kama Bandari VC na High Voltage hawatakuwa na mzunguko mzuri.
Kwa upande wa klabu za wananawake, Klabu ya Jeshi Stars ilihitimisha mzunguko wa kwanza ikiwa kinara kwa michezo mitano ambayo walishinda yote na kuvuna pointi 14, nafasi ya pili walikaa Tanzania Prisons pointi 13, michezo mitano wakishinda minne na kupoteza mmoja.
Wakati nafasi ya tatu kwa ukaribu, wapo Bandari VC na pointi zao 12 licha ya kushinda michezo minne kati ya mitano.
Swali sasa ni je, nani kumaliza vyema mzunguko wa pili na watatu hadi fainali?
Majibu yote yatapatikana pale TVF Arena, Mwembeyanga.
Ili kushuhudia magwiji wa mchezo huo, kila mpenzi anaombwa kwenda kutazama ‘smash' za maana kutoka kwa wakali na 'master wa setters.’ Ukiachilia kurejea kwa burudani hiyo pendwa kwa wapenda mpira wa wavu nchini, kurejea kwa mzunguko wa pili kulisindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki nchini Tanzania wakiwamo Simba Mwala na K-Zungu, ambaye ni mkali wa freestyle.
Mzunguko wa pili wa TVNL ulianza Septemba 6 na unatarajiwa kufika tamati Septemba 19 na kushuhudiwa mubashara kupitia Azam Sports 3 HD.
Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.
- Mpira wa wavu
- TVNL
- Mwembeyanga