Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Magereza wasema Lissu hajagoma, anakula kama kawaida

Jana ilitangazwa hadharani na mawakili wa mshitakiwa wa uhaini, Tundu Lissu, kwamba angeanza mgomo wa kula ili kushinikiza kupata haki ya kuonana na kuzungumza na mawakili wake ndani ya gereza bila kuingiliwa faragha. Soma zaidi Pambazuko kujua nini kinaendelea sasa.

Jumanne, 27 Oktoba 2026 · 14:21Dakika 1 kusoma
Lissu akiwa ndani ya mahakama
Lissu akiwa ndani ya mahakama — Picha kutoka Maktaba ya Pambazuko

JESHI la Magereza Tanzania limesema kuwa mahabusu Tundu Lissu linayemtunza ndani ya Gereza la Ukonga, Dar es Salaam, hajagoma kula.

Hivyo kukanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Lissu - anayeshitakiwa kwa kosa la uhaini, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameanza mgomo wa kula tangu jana.

Msemaji wa jeshi hilo, Elizabeth Mbezi, amesema leo kwamba taarifa hizo si za kweli, akisisitiza kuwa Lissu yupo salama na anaendelea vyema na maisha yake gerezani.

Mbezi pia amekanusha madai kwamba mawakili watatu wa Lissu wamezuiwa kumuona, akieleza kuwa wanaendelea kupata fursa hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu za Magereza.

Jeshi hilo limewataka wananchi kupuuza taarifa hizo na kujiepusha na kusambaza habari zisizothibitishwa, likionya kuhusu uwezekano wa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kauli hiyo imekuja siku tatu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Dkt. Rugemeleza Nshala, kueleza Oktoba 24, 2026, kwamba Lissu angeanza mgomo wa kula Oktoba 26, akipinga kile alichodai kuwa kunyimwa haki ya kuzungumza na mawakili wake kwa faragha.

Hata hivyo, bado kuna tofauti kati ya maelezo ya Magereza na madai yaliyotolewa na upande wa Lissu kuhusu utekelezaji wa haki hiyo.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • Lissu
  • mgomo wa kula
  • magereza

Soma Pia

Magereza wasema Lissu hajagoma, anakula kama kawaida | Pambazuko