Vituko vya Wakubwa
Maajabu ya Rais Mobutu akiwa Ikulu DRC - III
TUNAENDELEA simulizi na visa, vituko na mikasa vilivyofanywa na Rais wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), Mobutu Sesseseko Kuku wa Zabanga.

TUNAENDELEA simulizi na visa, vituko na mikasa vilivyofanywa na Rais wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), Mobutu Sesseseko Kuku wa Zabanga.
Huyu alikuwa kiongozi aliyechukua madaraka baada ya mapinduzi, miaka michache baada ya kifo cha rais wa kwanza baada ya wakoloni, Patrice Lumumba.
Mobutu, kwa lugha ya vijana, alikuwa ‘chuma’ kweli. Nani angethubutu kumnyoshea kidole katika zama zake?
Hata hivyo, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, hatimaye Mobutu aliyekuwa mtu wa ‘kula bata’ na mvinyo kutoka Paris Ufaransa, Monaco na Rabat alifika mwisho.
Siku chache kabla ya kuondolewa madarakani kupitia mapinduzi yaliyoongozwa na Laurent-Désiré Kabila, waliomshuhudia Mobutu - wa kansa ya korodani.
Kipindi ambacho urais wake uliingia kwenye majaribio ya kupinduliwa na uasi kuongezeka ni miaka ya 1992 hadi 1997, katika kipindi hicho urais wake haukuwa wa kula bata tena, kwani hata yeye mwenyewe aliona wazi kuwa “Zaire siyo mali yake tena.”
Ni kipindi ambacho hata askari ambao walikuwa watiifu kwake, walianza kumsaliti.
Mwaka 1986, Mobutu alianza kutetea ufalme wake, aliunda kikosi maalumu cha ulinzi wake binafsi kilichojulikana kwa jina la DSP, ambacho kilikuwa katili kwa kila aliyeshukiwa kuwa “mpinzani.”
DSP kilikuwa na wanajeshi wanaokadiriwa kufikia 10,000, huku wengi wao wakitoka kabila la Mobutu la Ngbandi. Wanajeshi hao walikuwa wanapewa mafunzo nchini Israel, pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa kabisa.
Ikumbukwe kuwa kabla ya Mobutu, Zaire iliongozwa na rais wake wa kwanza aliyeitwa Joseph Kasavubu, huyu alilindwa na mwanajeshi mmoja au wawili.
Mara nyingi alipokuwa akitembea hakuwa na msafara wowote.
Wanajeshi wa DSP walilipwa vizuri zaidi na Mobutu, na aliwaamini sana. Kila alipokwenda kuishi kijijini kwake ambako baadaye uligeuka kuwa mji, huko Gbadolite alisindikizwa na wanajeshi 300 ikiwa ni kwa ajili ya ulinzi tu.
Ijumaa ya Mei 16, 1997, Mobutu alinusurika kufa, wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Ndiji karibu na Kinshasa. Akiwa ndani ya ndege, dakika za mwisho ndege ianze kuruka, mkuu wa usalama wa Mobutu, Kanali Motoko alipokea taarifa ya kiintelijensia kuwa kwenye shamba kubwa lililokuwa karibu na uwanja huo kuna gari la jeshi aina ya jeep likiwa na vifaa vyote vya kudungulia ndege ya Mobutu.
- zaire
- drc
- mobutu
- vituko