Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Vituko vya Wakubwa

Maajabu ya Rais Mobutu akiwa Ikulu — IV

WAPENZI wasomaji, tunaendelea na simulizi ya visa, vituko na mikasa vilivyofanywa na Rais wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), Mobutu Sesseseco Kuku wa Zabanga.

Jumatatu, 21 Septemba 2026 · 06:00Dakika 4 kusomaToleo 183, uk. 32

Akiwa Brazaville, mwanawe Mobutu aliyeitwa Kongolu, alimpigia simu baba yake akimweleza kuwa wamekwama kupata hifadhi, Mobutu alituma ndege ya rais ikamchukue mwanawe, lakini ilipofika huko ilizuiliwa na Serikali ya Brazzaville, hivyo Mobutu akabaki bila ndege.

Ikabidi msaidizi wa mkuu wake wa ulinzi ajiongeze kwa kuiteka ndege ya Urusi iliyokuwa imeegeshwa pale uwanjani ili kumtorosha Mobutu kumpeleka Kinshasa.

Kwa nini Major Ngani aliiteke ndege ya Jeshi la Urusi wakati rais ana ndege yake? Jibu ni ndege, mwanawe aliyeitwa Kongolu Mobutu alikuwa tayari ameshakimbia nchi, alikimbilia Brazzaville, hivyo akiwa huko alimwambia baba yake kuwa wamekwama huko Brazzaville.

Mobutu kuona hivyo alituma ndege yake ikamchukue mwanawe, lakini iliyofika huko ilikataliwa na Serikali ya Brazzaville hivyo Mobutu alibaki bila ndege.

Ndio maana ilibidi msaidizi wa mkuu wake wa ulinzi aiteke ndege pale uwanja wa ndege ili kumtorosha Mobutu kumpeleka Kinshasa.

Mobutu aliingizwa kwenye ndege kubwa ya kivita yeye na gari lake kwa sababu zile ndege hazina viti, wakati inaruka, kikosi cha DSP kiliingia uwanja wa ndege na kumrushia mabomu na risasi, lakini walikwishachelewa.

Huku akiwa anaumwa sana na mwenye mawazo, Mobutu alimwambia daktari wake “hii siyo Zaire yangu tena, sina tena cha kuifanyia nchi hii.”.

Mobutu aliondoka mpaka Kinshasa, kisha akafanya maadalizi ya kuelekea Gbadolite kijijini kwake kisha akarejea Kinshasa, ambapo alikaa kwa muda mfupi kabla ya kutorokea Rome na baadaye Morocco ambako alikaa huko muda mfupi kisha akapoteza maisha kwa ugonjwa wa kansa ya kibofu ambapo alikufa akiwa na chini ya kilo 40.

Ikumbukwe kuwa Mobutu alikuwa ni kiongozi aliyeingia kijeshi huko Zaire. Mke wake wa kwanza Marie-Antoinette Mobutu, alifariki kwa ugonjwa wa moyo Oktoba 22, 1977 huko Genolier, Switzerland akiwa na umri wa miaka 36.

Lakini Mei 1, 1980, Mobutu alimuoa Bobi Ladawa pamoja na pacha mwenzake, Kosia.

Hawa walikuwa mapacha wanaofanana na aliamua kuwaoa wote.

Mobutu alitoka kabila la Ngbandi, watu kutoka eneo la kaskazini magharibi mwa Congo, Mobutu alizaliwa katika Mji wa Lisala Kongo, mama yake Mobutu Marie Madeleine Yemo, alikuwa mhudumu wa hoteli aliyekimbia kijijini kwao Lisala kwa vitisho vya chifu wa kijiji.

Alikutana na baba yake Mobutu Alberic Gvemani ambaye alikuwa mpishi wa jaji wa Kibelgiji. Jina la Mobutu alipewa na mjomba wake. Baba yake alifariki akimwacha Mobutu na umri wa miaka nane.

Mke wa jaji alihuzunishwa sana na kifo hicho na alijenga mapenzi makubwa kwa kijana Mobutu, alianza kumfundisha kuongea, kusoma na kuandika Kifaransa na hatimaye Mobutu alikua akiwa na uwezo mzuri wa kuzungumza lugha hiyo.

Mama yake aliyeitwa aliishi kwa kutegemea msaada wa ndugu na jamaa hali iliyomlazimu kuhama kila mara ili kukidhi mahitaji ya watoto wanne alioachiwa na marehemu mumewe.

Elimu ya kwanza ya Mobutu ilikuwa Leopoldville (Kinshasa ya sasa), lakini mama yake alimhamishia kwa kaka yake huko Coguilhaville, ambako alijiunga na shule ya Christian Brothers School, hii ilikuwa shule ya bweni chini ya Kanisa Katoliki.

Kutokana na umbo lake alikuwa maarufu katika michezo na masomo pia ambapo alichaguliwa kuwa mhariri wa gazeti la darasa lake.

Mobutu pia alijulikana kwa kuigiza wanafunzi wenzake. Wengi wanamkumbuka alivyokuwa anamwigiza padre Mbelgiji ambaye lugha yake ya kwanza ilikuwa Kiholanzi na alizungumza kifaransa kwa makosa.

Mwaka 1949 Mobutu alitoroka shule kwenda Leopoldville kukutana na rafiki yake wa kike aitwaye Attonete. Mapadre walipogundua hilo, walimkamata na mwaka wa shule ulipokwisha, Mobutu alipewa adhabu ya kutumikia jeshi kwa kosa la kutoroka shule. Hii ndiyo ilikuwa adhabu kwa wanafunzi watukutu.

Akiwa jeshini Mobutu alikutana na nidhamu katika maisha yake ya jeshini, hakujua kuwa kupitia jeshi angekuwa kiongozi mkubwa. Kiukweli Mobutu hakupenda jeshi, alipelekwa kama adhabu, lakini nafasi hiyo baadaye ndiyo ilimtambulisha duniani kote kama kiongozi ambaye ameacha alama ya machozi na machungu kwa Wacongomani.

Mobutu alifanya yote aliyotakiwa kufanya kwa nidhamu, pia alianza kuazima magazeti kutoka kwa maofisa Wabelgiji na vitabu kila alichoweza na alipenda kusoma kila alipopata nafasi.

Katika vitu alivyopenda kusoma ni makala na mada za Rais wa Ufaransa wa wakati huo, Charles de Gaulle, Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchil na mwana philosofia Muitaliano, Niccolo Machiavelli.

Akiwa mwandishi, Mobutu alikuwa akitumia jina bandia akiandika zaidi mambo yanayoendelea katika siasa nchini humo.

Akutana na Lumumba Mwaka 1955, Mobutu aliacha jeshi na kuwa mwandishi wa habari. Aliandikia gazeti la Leopoldiville daily L’Avenier.

Miaka miwili baadaye alikwenda Ubelgiji kuandika habari juu ya maonyesho ya 1958 World Exposition. Alibakia huko kupata mafunzo zaidi ya uandishi wa habari.

Muda huo Mobutu alishakutana na vijana wengi wa Congo, wasomi ambao walipinga utawala wa kikoloni.

Alianza urafiki na Patrice Lumumba na alijiunga na chama cha Lumumba cha Mouvement National Congolais (MNC).

Mobutu hatimaye aliteuliwa kuwa msaidizi maalum wa Lumumba ingawa watu walishaanza minong’no kuwa Mobutu anafanya kazi na shirika la ujasusi la Ubelgiji.

Makala haya ambayo yamepatikana kutoka vyanzo mbalimbali, yataendelea wiki ijayo.

  • Mobutu
  • Congo
  • Historia
  • Afrika

Soma Pia