Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Kutoka Kesi ya Lissu

Ushahidi wa simanzi kutoka kwa Heche

MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, ambaye ni shahidi wa Tundu Lissu katika kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wake huyo, ameweka wazi matukio ya kusikitisha.

Alhamisi, 17 Septemba 2026 · 10:31Dakika 4 kusomaToleo 182, uk. 22
John Heche (mwenye kofia) akiwa na Tundu Lissu kwenye picha ya kutengenezwa.
John Heche (mwenye kofia) akiwa na Tundu Lissu kwenye picha ya kutengenezwa. — Picha zote kutoka Maktaba ya Pambazuko

UMATI wa watu unaofuatilia ushahidi wa kesi ya uhaini katika Mahakama Kuu - Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, umepitishwa katika ushahidi wenye mnyororo wa matukio ya simanzi uliowahi kufanyiwa viongozi wa chama hicho.

Mwenye kubeba simulizi zaidi ya simanzi ni kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche wakati akiendelea kutoa ushahidi wake katika kesi inayomkabili mwenyekiti wake, Tundu Lissu.

Heche, shahidi wa tano katika kesi hiyo ametumia muda mwingi kuieleza mahakama namna ambavyo vyombo vya dola vimekuwa vikiwaandama viongozi na watu wa karibu wa viongozi hao, ikiwemo madai ya kuwakamata, kuwateka, kuwafungulia kesi na hata wengine kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.

Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini namba 19605/2025 iliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, ikiwa chini ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Jaji Dunstan Ndunguru. Majaji wengine ni James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Katika ushahidi wake alioanza kuutoa Septemba 9, 2026, Heche aliwaeleza majaji kuwa ameshiriki uchaguzi mara kadhaa akiwa mgombea ambapo amewahi kuwa diwani, mbunge na kushiriki kwenye kampeni za chama chake, lakini zote ziliambatana na maumivu makubwa.

Maumivu hayo ni pamoja na kutekwa, kuenguliwa kwa wagombea kwa kuambiwa hawajui kusoma na kuandika na kuibwa kwa fomu za viapo vya mawakala.

Heche ameipitisha mahakama katika simulizi za matukio hayo yenye simanzi akielekea kutoa ufafanuzi wa msimamo wa chama wa “No Reform No Election” ambapo alieleza kuwa ilimaanisha kuweka msukumo kwenye mabadiliko ya kimfumo hasa katika kusimamia uchaguzi huru na wa haki, kuanzia kwenye muundo wa tume ya uchaguzi.

Alieleza mahakama jinsi alivyokamatwa akiwa Tarime na kufikishwa Dar es Salaam Novemba 4, 2025 ikiwa ni siku chache baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, baada ya kupitishwa Dodoma na kufikishwa Dar es Salaam, ambapo katika Kituo cha Polisi Oysterbay, aliwakuta mawakili wa serikali Nassoro Katuga, Job Mrema, Thawabu Issa na Cathbert Mbilinyi.

“Siku hiyo kulikuwa na watu wengi sana pale kituoni ambao walikuwa wamekamatwa, wengine wakiwa wamejeruhiwa…”

“Niliambiwa walikuwa wamekamatwa kwa sababu ya vurugu za uchaguzi. Waliwekwa kwenye selo zao hadi kwenye korido. Hawa mawakili walikuwa pamoja na George Bagemu.

“Nilipelekwa kwenye chumba ghorofa ya kwanza na kusomewa kwamba ninakabiliwa na kosa la ugaidi, nikidaiwa kuhusika na kuchoma vituo vya mwendokasi kuanzia Kimara hadi Ubungo…”

“Sikuwa tayari kuandika maelezo yangu. Walichukua tu majina yangu na mahali ninapoishi, kisha baada ya hapo wakanipeleka Kituo cha Polisi Mburahati ambapo niliwekwa humo kwa siku saba,” alisema.

wa, pia mwanachama wao Akwilina Akwilini, ambaye Polisi ilikiri aliuawa kwa risasi na hakuna aliyekamatwa wala kushitakiwa.

Badala yake, alishitakiwa yeye na wajumbe wa kamati kuu ya chama chake, akiwemo John Mnyika, ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu; Freeman Mbowe ambaye alikuwa Mwenyekiti; Vincent Mashinji aliyekuwa Katibu Mkuu; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini.

Wengine ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar kwa makosa ya uchochezi na kushiriki kusanyiko lisilo na kibali.

Heche aliipitisha mahakama katika shambulio la risasi dhidi ya mwenyekiti ambaye kwa sasa anakabiliwa na shitaka la uhaini, Lissu ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti na kulazimika kupatiwa matibabu nje ya nchi, kisha wao kuhukumiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini inayofikia shilingi milioni 300.

Alieleza kuhusu mauaji ya Alphonce Mawazo, ambaye alikuwa mgombea wa Jimbo la Busanda mwaka 2015 na mwenyekiti wa chama chake Mkoa wa Geita na kwamba wakati akifunga kampeni Nyamongo mwaka 2020, walivamiwa kwa risasi, ambapo watu wawili, Chacha Isangora na Chacha Gabir waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Alisema akiwa katika shughuli za siasa, mdogo wake, Suguta Heche aliuawa ambapo awali alikamatwa Sirari mwaka 2018, akafungwa pingu mikono nyuma na kuchomwa sindano akiwa katika hali hiyo.

Heche alieleza baada ya tukio hilo, kulikuwa na madai ya jaribio la kumtupa ili ionekane amepata ajali au ameshambuliwa na watu wasiojulikana, lakini walinzi wa eneo waliona kilichokuwa kinaendelea, hivyo akarudishwa kituo cha polisi.

“RPC wa wakati huo alitoa taarifa kwa umma kwamba mdogo wangu ameuawa kikatili na kwamba hatua zingechukuliwa. Askari aliyekuwa anahusishwa na tukio hilo aliachiliwa na kuhamishwa kituo, na mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.

“Ninaamini mdogo wangu aliuawa kutokana na msimamo wangu wa kisiasa na kupinga maovu ya nchi hii, na kwamba tukio hilo lilikuwa ujumbe kwamba wanaweza kufanya lolote bila hatua za kisheria kuchukuliwa,” aliieleza mahakama.

Alisema kumekuwa na matukio ya kukamatwa kwa Lissu kwa kesi za uchochezi ambazo alizofunguliwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 ambazo ziliisha tu ambapo baadhi yake ilisemekana serikali haikuwa na nia ya kuziendeleza.

Alieleza kuwa mara kadhaa ratiba zao zimeingiliwa na polisi, watu kupigwa kwenye mikutano ya kampeni, wagombea kunyimwa fomu za matokeo, kura za uongo kuingizwa kwa maboksi na mabegi na askari polisi ambao walitakiwa kusimamia uchaguzi.

Heche ambaye wakati wote aliongozwa na Lissu, mtuhumiwa anyejitetea mwenyewe akisaidiwa kwa karibu na jopo la mawakili wake, alieleza kuwa katika uchaguzi wa Arumeru, aliyekuwa katibu wa USA River, Msafiri Bwambo, aliuawa kwa kuchinjwa kwa msumeno na watu waliosadikiwa kuwa wanachama wa CCM.

Alisema kwa Dar es Salaam, Kinondoni, Mwenyekiti wa Chadema Ananasi, Dani Yona aliua- Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, akiwa Mahakama Kuu - Masijala Ndogo ya Dar es Salaam baada ya kumaliza kumuongoza shahidi wake wa tano, makamu mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, mwishoni mwa wiki.

  • lissu
  • uhaini

Soma Pia