Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Tafakuri ya Bagonza

Ukakasi na uhaini mamboleo

KAMA ilivyo na ukakasi kuzoea kumuita rais “mama au baba,” inaweza kuwa na ukakasi kumwita makamu war ais; “mtoto au mwanetu.”

Jumatatu, 31 Agosti 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 180, uk. 10
Askofu BDkt. enson Bagonza
Askofu BDkt. enson Bagonza — Picha kutoka Maktaba ya Pambazuko

Rais ni rais bila kujali jinsi yake. Makamu ni makamu bila kujali umri wake. Katika umri wa miaka 38, Nilikataa kuitwa “askofu mtoto” ili watu wasitumie utoto wangu kulihujumu kanisa.

Nakubali, hakuna shule ya urais au umakamu, lakini pia nchi siyo ya kufanyia mazoezi ya kuongoza. Nimewasikia watu kadhaa wakiwabeza wapinzani kuwa hawana uzoefu na kwamba nchi siyo ya kufanyia majaribio.

Uteuzi wa Makamu wa Rais wa Tanzania, Deo Ndejembi umemaliza kijembe hicho. Mtu yeyote, kijana, mzoefu, mpinzani, msomi, asiyesoma, anaweza kuongoza akiwa na utashi.

Namtakia Ndejembi kila jema. Amebeba dhamana kubwa katikati ya miiba. Asiuone ujana kama mtaji. Auone Umakamu kuwa mtaji.

Kinachosumbua vichwa vya wengi siyo umri wala makolokocho mengine. Ni namna ya kuingia na kutoka. Mtindo huweka kanuni isiyoandikwa.

Tumelazimishwa kulizoea neno “uhaini.” Sasa tuna uhaini mamboleo. Uhaini una sura nyingi. Kuna haja ya kuliangalia hili neno kikatiba. Upo uhaini dhidi ya serikali. Upo pia uhaini dhidi ya wananchi.

Siyo wakati wote uhaini dhidi ya serikali ni uhaini dhidi ya wananchi. Siyo wakati wote uhaini dhidi ya wananchi ni uhaini dhidi ya serikali.

Upo uwezekano wa serikali na wananchi kutokuwa kitu kimoja na hivyo kuwezekana kufanyiana uhaini. Tumewalazimisha wananchi wengi waonekane ni wapinzani.

Ufa kati ya matajiri na maskini ni mkubwa sana. Ufa kati ya wananchi na serikali ni mkubwa mno. Haya mawili yanadai uongozi siyo utawala. Siyowakati wote, mtawala anakuwa ni kiongozi.

Nakusihi msomaji usijifanye kuwa Mjaluo. Tafakari kabla hujanifanya kuwa mhaini. Jipe muda ili nisikuone wewe ni mhaini dhidi yangu.

Mwandishi wa safu hii ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe. Ni mchangiaji maalum wa safu na makala ndani ya Pambazuko.

  • Uhaini
  • Deogratius Ndejembi
  • Utawala

Soma Pia