Habari Kuu
Yaliyojificha nyuma ya simu za mkopo
HIVI sasa ukipita katika maeneo mengi yenye misongamano mijini, lazima ukutane na kelele za matangazo ya simu za mkopo.

Mbali na kuwa na maduka, wakopeshaji wa simu za mkononi wengine wameegesha vibanda wakitangaza kuwa na huduma hiyo kama wanavyofanya baadhi kwa kuchomeka miamvuli kwenye meza na kugeuza kituo cha kukopesha simu.
Hawa wote huwavuta zaidi watu wenye kipato cha chini, kuchangamkia ‘fursa’ hii, wakiamini katika masharti ambayo kwa “haraka-haraka” yanaonekana kuwa nafuu sana, lakini ukizama kwa ndani yana maumivu makubwa kwa wakopaji.
Kuna mengi yaliyojificha katika ‘biashara’ hii inayozidi kukua kila siku katika miji mikubwa hasa Dar es Salaam.
Mathalan, wakati wakopeshaji hawa wakionyesha kuwa gharama za kupata simu ni ndogo – wao wanaiita kianzio, lakini ukikokotoa hesabu ya fedha zote mteja anazolipa hadi anakamilisha kulipa deni lake la simu, unabaini kuwa simu hiyo inakopeshwa hadi mara mbili hadi tatu ya thamani yake halisi iwapo itanunuliwa kwa fedha taslimu.
Masharti magumu zaidi
Gharama hiyo imejificha katika riba ya mkopo huo ambao hulipwa kupitia makato ya kila siku au wiki na masharti magumu ya umiliki wa kifaa hicho kabla ya mteja hajamaliza deni.
Kati ya masharti ambayo mkopaji anatakiwa kuyakamilisha ili kustahili kukopeshwa simu ni kuwa na kitambulisho cha taifa, mdhamini mmoja na kianzio kutegemea na aina ya simu. Lakini akishakopeshwa simu, anatakiwa kuanza kulipa deni hilo ndani ya wiki moja!
Matakwa ya sheria Haya yanatokea wakati serikali imeshatunga sheria mahususi kusimamia masuala ya mikopo.
Hii ni Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha (Microfinance Act, 2018) ambayo ndiyo sheria kuu inayosimamia taasisi zote zinazotoa mikopo midogo.
Hawa wanaotoa mikopo ya simu wanaangukia katika uratibu na usimamizi wa sheria hii.
Sheria hiyo inataka kila mtoa mkopo kuwa na leseni halali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inayomruhusu kufanya shughuli hiyo na kwamba kutoa mkopo bila kibali ni kosa la kisheria.
Pia Kanuni za Ulinzi wa Mtumiaji wa Huduma za Fedha (BoT Financial Consumer Protection Regulations), zinalinda wakopaji dhidi ya riba na tozo zisizoeleweka, udanganyifu au masharti ya siri.
Vilevile zinataka wakopeshaji waeleze wazi riba, ada zote na masharti ya mkopo kwa mtu anayehitaji mkopo.
Hata hivyo, pamoja na matakwa hayo ya sheria, uchunguzi uliofanywa na Pambazuko kwa miezi kadhaa sasa umebaini kuwa wakopeshaji wengi hawafuati masharti haya ya kisheria na kikanuni.
Uchunguzi umebaini kuwa wengi wa wakopeshaji simu hujipangia riba zao wenyewe na masharti yao ambayo baadhi yake hayaendani na matakwa ya sheria na kanuni.
Ufuatiliaji uliofanywa na Pambazuko kwa kujifanya ni mteja anayetaka kukopeshwa simu, umebaini kuwa wakopeshaji wengi hawako wazi kwa wateja kuhusu riba, tozo na adhabu za kukiuka masharti ya mikopo yao, jambo linalowaumiza wananchi wengi wanaokopa simu hizo.
Maumivi kwa wakopaji Uchunguzi uliofanywa na Pambazuko, umebaini kuwa kwa mfano simu yenye thamani ya Shilingi 450,000 kwa fedha taslimu inaweza kumgharimu mteja zaidi ya Shilingi 800,000 baada ya kumaliza makato ya kila siku au wiki kwa mwaka mzima.
Chini ya utaratibu waliojiwekea wengi wa wakopeshaji simu hao, mteja hulazimika kulipa kwa mujibu wa makubaliano na muuzaji na pale anapokiuka masharti anafungiwa simu hadi atakapofanya malipo.
Kwamba simu haitakuwa mali ya mteja hadi malipo ya mwisho yatakapokamilika na wakati wote mkopeshaji anakuwa ndiye mdhibiti wa simu husika kiteknolojia.
Mara nyingi, mtu akishindwa kulipa ndani ya muda simu yake hufungiwa na mkopeshaji.
Hali hiyo ya mkopeshaji kuwa na udhibiti wa simu kunatia hofu baadhi ya wakopaji wakihisi kuwa mkopeshaji huyo anaweza pia kuingilia au kuangalia taarifa na data zao nyingine kwenye simu.
Wananchi wengi wamekuwa na hofu kuhusu usalama wa taarifa zao hasa baada ya muuzaji kuwa na uwezo wa kuifunga simu isitumike licha ya kwamba haipo katika himaya yake.
Vilevile, pamoja na sheria kukataza lakini kumekuwa na malalamiko kuhusu riba kubwa na masharti yasiyo ya wazi.
Isack Tarimo, Mkazi wa Sinza-Dar es Salaam, ambaye ni miongoni mwa waliokopa simu hizo, ameliambia Pambazuko kuwa wakopeshaji wengi hawatoi elimu kwa wateja wao kuhusu riba na masharti mengine.
“Hizi simu tunazikopa kwa vile tuna kipato kidogo. Kwa mfano sisi madereva wa bodaboda, hauwezi kuwa na laki mbili au tatu kwa wakati mmoja, ndio maana tunakimbilia huko kwenye mikopo...”
“Hata hivyo, ingawa inaonekana ni nafuu kukopa lakini ni mateso...”
“Mtu unalipa tu kila siku au kila wiki, kuna wakati hata hujui jumla umelipa kiasi gani maana hakuna uwazi,” amesema.
Tarimo pia ameeleza wasiwasi wake kuhusu wakopeshaji wa simu hizo kuingilia mawasiliano yake.
“Mimi nimekopa tangu Januari na kwa siku narejesha Shilingi 2,700 nilichukua simu aina ya Infinix Smart 20 ambapo kwa fedha taslimu inauzwa Shilingi 380,000. Lakini nilipopiga hesabu nimebaini kuwa hadi nitakapomaliza deni nitakuwa nimelipa zaidi ya shilingi laki saba...”
“Kinachokera ni kwamba yaani ukichelewa tu kidogo kupeleka rejesho la siku unakuta simu imefungwa ghafla na huwezi kufanya chochote. Sasa kama wana uwezo wa kufanya haya hawawezi kuingilia mawasiliano yangu kweli?” anahoji.
Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca), 2010; ambayo iko chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ndiyo sheria kuu inayolinda faragha ya taarifa za mteja, kuzuia matumizi mabaya ya huduma za simu na kuweka wajibu kwa kampuni za simu kuhakikisha usalama wa huduma.
Pia mwaka 2022, Bunge lilipitisha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (The Personal Data Protrction Act, 2022), ambayo imeanza kutumika kulinda faragha na usalama wa taarifa za wananchi na inasimamiwa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).
Kwa kuzingatia umuhimu wa sheria hizo, Pambazuko lilimtafuta Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa (TCRA), Rolf Kibaja, ambapo alisema mamlaka hiyo haihusiki na chochote kuhusu simu hizo za mikopo.
“TCRA haihusiki kabisa watafute watu wa taasisi inayohusika na taarifa binafsi… sisi kwenye simu hizo za mkopo hatuhusiki,” amesisitiza Kibaja.
Tume ya Ulinzi yanena Gazeti hili likamfikia Ofisa Habari wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Evelyne Urio, ambapo amesema hadi sasa hawajapata malalamiko yoyote kutoka kwa watumiaji wa simu hizo.
Pia amefafanua kuwa inategemeana na mikataba waliyokubaliana kati ya muuzaji na mtumiaji.
“Kwa mfano labda wamekubaliana kwamba mteja akikiuka masharti labda picha na details wanaziweka hadharani sasa kama waliandikishiana sisi hatuwezi kuingilia hilo...”
“Lakini kama anayekopesha kaenda kinyume na makubaliano sisi hapo ndio tunahusika na kumchukulia hatua,” amesema.
Victoria Urassa, muuzaji wa simu hizo katika eneo la Kariakoo, akizungumzia utaratibu wa kumfungia simu mteja asipofanya marejesho, anasema kuna mfumo ambao wanauweka kwenye simu.
“Hata usipolipa ikipita ile tarehe automatically simu yenyewe inajifunga, yaani huwezi kufanya chochote,” amefafanua.
Akielezea kuhusu hofu ya wateja kuwa wanaweza kuingiliwa faragha, Ahmed Khamis ambaye ni mkopeshaji wa simu hizo eneo la Makumbusho, anasema mfumo wa kukopesha unadhibiti uhuru wa simu kwa mtumiaji.
Anaongeza; “Jinsi mfumo ulivyowekwa simu yako huwezi kuifuta, lakini kuhusu kuingilia sijui kusoma meseji za mteja siyo kweli... wanahofu tu lakini hakuna kitu kama hicho.”
Lema (pichani), aliwahi kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema wananchi wanadanganywa na wakopeshaji wa simu huku serikali ikiwa imekaa kimya.
nanchi, Shilingi 100,000 zinakuwa Shilingi 240,000 kwa mwaka kutokana na takribani riba ya asilimia 20 kila mwezi…”
ashangaza BoT imekaa kimya, ikiruhusu wananchi kuangamia kifedha kwa uzembe wao,” aliandika Lema.
BoT yawaonya Kuu ya Tanzania (BoT), Innocent Mmari, ameliambia Pambazuko kuwa mfumo wa ukopeshaji kwa simu unasimamiwa na BoT na kwamba mtoa huduma lazima awe amesajiliwa.
kama Tier 2 Microfinance Service Provider na apate pia No Objection letter kabla ya kutoa huduma za mikopo,”amesema Mmari.
Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbles “Mikopo ya simu imegeuka kuwa fataki kwa wa- “Hii siyo mikopo bali ni kudanganya raia, in- Ofisa Itifaki na Uhusiano wa Umma wa Benki “Mtoa huduma lazima awe na leseni kutoka BoT Hata hivyo, wakopeshaji simu kadhaa waliotembelewa na Pambazuko hawakutaka kuonyesha Alipoulizwa kama mikopo hiyo ni ya kidigitali, Mmari amesema: “Guidance Note inafafanua mkopo wa kidigitali kuwa mkopo ambao maombi, uidhinishaji, utoaji na marejesho yake yanafanyika kupitia njia za kidigitali kama vile simu ya mkononi, program (App), tovuti au majukwaa mengine ya kidigitali.”
Kuhusu kikomo cha riba, amesema mwongozo unataka riba, ada, gharama zote, adhabu za kuchelewa kulipa, muda wa mkopo na masharti mengine yaonyeshwe wazi kwa mteja kabla hajachukua mko- Katika hilo, akasisitiza kuwa mtoa huduma Akizungumzia kuhusu ulinzi wa mteja, amesema mwongozo umeweka masharti ya kulinda taarifa binafsi za wateja kwa kuzingatia Sheria ya Ulinzi wa Taaifa Binafsi ya mwaka 2022.
“Kuzuia wakopeshaji kufikia contact list, sms, picha, email au taarifa nyingine zisizohitajika za mteja. “Kuzuia vitisho, unyanyasaji, aibu ya hadharani au kutuma ujumbe kwa ndugu na marafiki wa mteja kwa lengo la kumdhalilisha, kutaka taarifa za gharama za mkopo ziwekwe wazi, kuweka njia rasmi za kupokea malalamiko ya wateja,” amesema alipotakiwa kutaja baadhi ya masharti hayo.
Kuhusu wauzaji wanaokwenda kinyume na sheria ya BoT, Mmari amesema wanachukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kusimamishwa kwa majukwaa yasiyo na leseni au yasiyotii maelekezo ya BoT.
“Hata wale ambao wanaendesha majukwaa bila No Objective Letter ya BoT nao tunawachukulia hatua kali,” amesisitiza Mmari.
Simu hazina ubora Gazeti hili limebaini pia asilimia kubwa ya simu hizo kutokuwa na ubora ambapo mwanzoni mteja anaponunua inakuwa haina tatizo, lakini kadiri anavyotumia huwa inazimika mara kwa mara.
Josephat Eliud mkazi wa Makabe-Mbezi, ambaye ni miongoni mwa waliokopa simu hizo ameliambia Pambazuko kuwa wanapata changamoto kwani simu hizo zimekuwa hazina ubora.
“Mara nyingi wanatukopesha simu ambazo siyo nzuri huku nyingi zikiwa na matatizo. Simu unachukua leo baada ya siku chache tu inaanza kusumbua...” “Cha kusikitisha ni kwamba hata ukirudisha simu kwa ajili ya matengenezo, unaweza kuambiwa uiache hapo itengenezwe, halafu uchukue baada ya siku tatu au zaidi. “Hii inatuathiri sana kwa sababu simu ni kifaa muhimu kwa mawasiliano na shughuli zetu za kila siku,” amesema.
Amesema mbali na matatizo hayo, gharama wanazotozwa ni kubwa sana, hivyo wanahisi kuna udanganyifu au ukosefu wa uwazi. Kutokana na hilo, ameiomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli na kulinda haki za wateja.
Maduka ya ‘cash’ hoi Katika ufuatiliaji wake Pambazuko limebaini kuwa wafanyabiashara wanaouza simu kwa pesa taslimu sasa hawapati wateja wengi kwani wateja wengi wanakimbilia kwenye simu za mikopo.
Wachumi waliozungumza na Pambazuko wamesema hilo linatokana na ugumu wa hali ya maisha.
“Mtu anaona afadhali alipe simu kidogo kidogo kwani hana fedha nyingi taslimu za kununua simu.
Hata akijua kuwa mwishowe atalipa fedha mara dufu lakini kule kulipa kidogo kidogo kunampa nafuu kwa sababu kipato chake ni kidogo,: anasema mchumi mmoja.
Wakizungumza na Pambazuko kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wa simu wamesema tangu biashara ya simu za mikopo zilipoanza wamekuwa na hali mbaya.
“Yaani unaweza kukuta siku nzima nimepata mteja mmoja au kuna wakati hakuna hata mmoja, imefika hatua wenzangu wengine imebidi na wao waanze kuuza kwa mikopo.
“Mimi hapa nimeajiriwa lakini naona dalili ya bosi kufunga duka maana hali ni mbaya,” amesema Pendo Cosmas, anayeuza duka la simu eneo la Mwenge.
Kelele za matangazo Changamoto nyingine ambayo gazeti hili limebaini ni kelele za spika zinazoshindana kutangaza biashara hiyo ya kukopesha simu.
Baadhi ya maeneo yenye misongamano ambayo yameshamiri kwa kelele za spika katika Jiji la Dar es Salaam ni Kariakoo, Mwenge, Manzese, Makumbusho, Bunju B na Tegeta.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewahi kueleza kuwa vyanzo vya kelele mijini vinahitaji kudhibitiwa kupitia matumzi sahihi ya ardhi, vibali kutoka mamlaka husika na matumizi ya vifaa vya kudhibiti sauti.
Changamoto za kelele, inasimamiwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni za Udhibiti wa Kelele na Mitetemo za mwaka 2015.
Sheria hiyo inapiga marufuku uzalishaji wa sauti kubwa zinazozidi viwango vinavyoruhusiwa katika maeneo ya makazi, biashara, karibu na taasisi za kijamii.
- Simu za mkopo
- Riba
- Walaji