Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Mitindo & Urembo

Adolphine, mumewe walivyotikisa kwenye vazi la asili la harusi

MWANAMITINDO na mjasiriamali, Adolphine Manywa, akiwa na mwenza wake wameteka hisia za wengi baada ya kuonekana wakiwa kwenye mavazi ya kipekee ya harusi ya asili.

Jumatatu, 31 Agosti 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 180, uk. 35
Adolphine Manywa, akiwa na mwenza wake
Adolphine Manywa, akiwa na mwenza wake — Picha kutoka mtandao.

Wawili hawa wameleta mapinduzi makubwa kwa kuchanganya utamaduni wa mwafrika na ubunifu wa kisasa uliowafanya waonekane kama mfalme na malkia kamili.

Bibi harusi amevaa gauni la lililopambwa kwa ushanga wa asili. Gauni hilo lina muundo wa ngozi ya ng'ombe kwenye sehemu ya kifuani na chini.

Amekamilisha muonekano wake wa malkia kwa kofia ya asili ya kusuka iliyopambwa pamoja na pepeo la mkononi lililotengenezwa kwa ngozi ya ng'ombe.

Kwa upande wa bwana harusi, amevaa suti ya rangi ya cream iliyowekwa kipande cha ngozi ya ng'ombe kifuani upande mmoja kinachoendana kabisa na gauni la bibi harusi.

Akaongeza na nakshi za kifalme kwa kuvaa kofia ya crown ya ngozi ya ng'ombe, miwani nyeusi, pamoja na bakora ya mfalme iliyochongwa kwa mti mweusi.

  • Mitindo
  • Harusi
  • Adolphine Manywa
  • Utamaduni

Soma Pia