Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Mitindo & Urembo

Gauni la Maua Sama lilivyoteka hisia

MWANAMUZIKI Maua Sama ameteka hisia za mashabiki na wapenda mitindo mtandaoni baada ya kuonyesha muonekano wake wa gauni akiwa mjamzito.

Jumatatu, 7 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 181, uk. 35

Maua Sama ambaye tayari amejifungua, alionyesha ubunifu wa hali ya juu uliounganishwa na urembo kupitia gauni lake maalum.

Gauni hilo ambalo ni la muundo wa samaki na lisilo na mikono, limeshika mwili na tumbo lake likiwa katika muonekano nadhifu.

Vazi hilo pia lina nakshi za vipande vya mng’ao sehemu ya juu na limetengenezwa kwa kitambaa cha uwazi cha rangi ya mwili, kilichotiwa nakshi za kioo na mawe ya mng’ao zilizopangwa kwa mchoro ya ming’ao ya kipekee kifuani.

Ili kuongeza urembo amevaa mikufu ya fedha ya chuma ambayo imewekwa kwa ulinganifu kifuani na tumboni.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • Mitindo
  • Maua Sama

Soma Pia