Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Kilinge cha Mawasiliano

AI imezungumzwa Mount Meru, Karatu hawajui chochote

IJUMAA asubuhi pale Mount Meru Hotel, Arusha, nilikuta watu wamevaa suti kali, walikuwepo maprofesa, madaktari wa falsafa, wamiliki wa kampuni za teknolojia na maofisa wa serikali.

Jumatatu, 28 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 184, uk. 24

Wote walikuja kwa ajili ya Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Utalii Arusha (AITC 2026), ulioandaliwa na Taasisi ya Uhasibu Arusha.

Kaulimbiu ilikuwa nzito; ‘Ajenda ya Kidijitali na Akili Mnemba Kuusanifu Upya Utalii.’ Nilipokea kitabu cha muhtasari wa tafiti 12.

Nikakisoma kama mzazi anayesoma matokeo ya kidato cha nne ya mwanawe. Kwa makini na kwa hofu kidogo.

Nikiwa nakunywa chai nilimkumbuka rafiki yangu mmoja, dereva na mwongoza watalii kutoka Karatu, kijana mjanja, anamjua kila simba wa Ngorongoro kwa jina lake la utani.

Nikajiuliza kama huyu bwana anajua kwamba leo hapa kuna watu wanajadili hatma ya kazi yake, jibu lake lilikuwa hajui.

Dkt. Anagrolia Mahenge anatuambia kwamba ‘safari janja’ haiji kwa kununua programu tu, inahitaji watu, taasisi, data, miundombinu na uongozi kukua pamoja.

Winniefrida Ngowi na Goodluck Abayo wamewahoji wadau 392 wa utalii kutoka Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Wamegundua kwamba fedha za kijani zinachochea matumizi ya Akili Mnemba.

Jacquiline Ndanu anasema ujuzi wa kidijitali wa wafanyakazi wetu wa utalii uko wastani wa 3.41.

Watafiti wa Mwenge Catholic University na wenzao wa Ubelgiji na Ujerumani wameorodhesha maeneo 38 ya kijiolojia kwenye miteremko ya kusini ya Mlima Kilimanjaro.

Kuna maporomoko ya maji, chemchemi, mabonde na vilima. Ni hazina ambayo huenda hata wanakijiji wanaoishi pembeni yake hawaioni kama hazina.

Vijana wa YoPal nao wanajenga jukwaa la usafiri kwa mikono ya Kitanzania, lenye msaidizi wa akili bandia anayeongea Kiswahili na Kiingereza.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • AI
  • Teknolojia
  • Kilimo
  • Karatu
  • Arusha

Soma Pia