Habari
Ajali ya chopa yakatisha uhai wa Chivayo, mkewe
Taarifa za kifo cha bilionea wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, sasa zimethibitishwa baada ya jana kuwepo sintofahamu kuhusu ajali ya chopa iliyotokea jioni.

BILIONEA maarufu wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, mkewe Lucy Muteke na watu wengine wanne, wamefariki dunia katika ajali ya helikopta (chopa).
Helikopta hiyo ilianguka jana - Septemba 30, takriban dakika 40 baada ya kupaa kutoka Gandami, Chikomba, ambako wanandoa hao walikuwa wakisimamia ujenzi wa nyumba yao ya kijijini.
Mamlaka za Serikali ya Zimbabwe na familia ya mfayabiashara huyo zinaeleza kuwa chopa hiyo ilianguka jioni ya katika eneo la Marondera. Hakuna sababu zilizotolewa kuhusu ajali hiyo iliyotawala vyombo vya habari duniani.
Msemaji wa Serikali ya Zimbabwe, Nick Mangwana, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema hakuna aliyenusurika katika chopa hiyo iliyokuwa na abiria sita.
Polisi wamesema ajali hiyo ilitokea karibu saa 11 jioni kwa saa za Zimbabwe na kwamba maelezo zaidi yangetolewa baada ya wahudumu wa dharura kufika eneo la tukio.
Chivayo amekuwa bilionea mwenye kutajwa zaidi kupata utajiri wake kwa njia zinazoelezwa kuwa tata, huku akionekana kuwa na ukaribu mkubwa na viongozi wengi wa Afrika Mashariki na Kati.
- ajali
- chopa
- chivayo
- bilionea
- zimbabwe