Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Ally Edha ahimiza kulipa kodi, kusaidia zaidi wahitaji

Wafanyabiashara pamoja na kuchangia maendeleo ya Tanzania, wamehimizwa kusaidia familia zenye uhitaji mkubwa zaidi na zenye kukabiliwa na changamoto za maisha, kama anavyofanya Ally Edha.

Jumatano, 7 Oktoba 2026 · 19:57Dakika 2 kusoma
Ally Edha Awadh
Ally Edha Awadh — Picha kutoka Maktaba ya Pambazuko

MWENYEKITI wa Lake Group, Ally Edha amewaasa wafanyabiashara kwamba pamoja na kulipa kodi, ni muhimu zaidi kujali watu wenye uhitaji na wanaoishi mazingira magumu.

 Edha ametoa rai hiyo juzi baada ya kumtembelea mama mmona  ambaye hakujitambulisha kwa jina, anayeishi katika mazingira magumu ya porini yanayohatarisha maisha yake kutoka kwa wanyampori, lakini bado akiwa na furaha na matumaini ya maisha.

 Mfanyabiashara amesema kuwa ni muhimu kulipa kodi ili kuchochea maendeleo ya jumla ya Tanzania, lakini kuna thawabu zaidi kunusuru kaya maskini.

 Kutokana na hilo, mfanyabiashara huyo ameanza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya mama huyo, baada ya kuguswa na hali ya maisha aliyokutana nayo wakati alipomtembelea.

 Akizungumza baada ya ziara hiyo, Ally amesema aliguswa na namna mama huyo anavyokabiliana na changamoto za maisha, huku akiendelea kuwa na matumaini na kushukuru kwa kile kidogo alichonacho.

 “Nimeguswa sana na huyu bibi, kweli amenigusa moyo wangu. Sisi wafanyabiashara tuna wajibu wa kisheria kulipa kodi, lakini vilevile tuna wajibu wa kuwasaidia watu. Tayari nimeleta mafundi, kesho waanze,” amesema Ally.

 Amesema maisha ya mama huyo yamemfundisha kuwa hata katika mazingira magumu, mtu anaweza kuendelea kuwa na matumaini na kuthamini alichonacho.

 “Ameonyesha kwamba hakuna kitu kama matumaini na kushukuru kile kidogo ambacho anacho. Nani alitegemea tungefika pale kwenye kijumba chake na kumsalimia, halafu baada ya kipindi kifupi mama huyu atakuwa na nyumba bora?” amesema.

Ally amesema wafanyabiashara wanapofanikiwa wana wajibu  kuwasaidia watu wenye uhitaji, akisisitiza kuwa mafanikio hayapaswi kuishia katika kulipa kodi na kutoa ajira pekee.

 “Wafanyabiashara unapobarikiwa siyo tu uwe unalipa kodi na kutengeneza ajira, bali tuna wajibu binafsi wa kuwatazama walioko chini yetu,” amesema.

 Aidha, Ally amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira yanayowawezesha wafanyabiashara kufanya biashara kwa wigo mpana.

 “Ninapenda kumshukuru mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kufanya biashara kwa uwanda mpana, ndiyo maana unapofanikiwa tunawakumbuka walioko chini yetu…”

 “Bila mheshimiwa rais tusingefika tulipofika. Zamani tulikuwa tunakimbia nchi, lakini tunapopata fursa tunakuwa malaika,” amesema Ally.

  • lake oil
  • msaada
  • kodi
  • edha
  • ally

Soma Pia