Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari

Dar yajipanga kukabili El-Niño

ya kutosha ya kupeleka maji kwenye mito au baharini,” alisema Chalamila wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Sa- MKOA wa Dar es Salaam umeanza kuchukua hatua za maandalizi ya kukabiliana na madhara yatakayotokana na mvua za El-Niño, zinazotarajiwa kuanza kunyesha mwezi ujao – Oktoba.

Jumatatu, 21 Septemba 2026 · 06:00Dakika 4 kusomaToleo 183, uk. 20

Akizungumza wiki iliyopita, mkuu wa mkoa huo, Albert Chalamila, alitaja baadhi ya maandalizi hayo kuwa ni kusafisha na kupanua mito na mifereji, kuboresha njia za maji na kuimarisha miundombinu katika maeneo hatarishi.

Maandalizi hayo yanakuja wakati kumbukumbu za mvua kali za El-Niño za 2023/24 bado zikiwa hai, baada ya mafuriko na maporomoko ya udongo kusababisha vifo, kuharibu barabara na madaraja na kuathiri shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa Dar es Salaam, changamoto kubwa ni namna ya kuyatoa kwa haraka maji mengi yanayokusanyika katika jiji wakati wa mvua kubwa na kuyaelekeza kwenye mito na hatimaye baharini.

“Moja ya changamoto ni kutokuwa na mifereji Alisema mkoa unahitaji kuendelea kujenga na kuboresha njia za maji, huku mito na mifereji iliyopo ikisafishwa na kupanuliwa ili kuongeza uwezo wa kupokea maji wakati wa mvua kubwa.

Dar yahitaji zaidi ya miundombinu Utupaji holela wa taka, ujenzi holela na shughuli nyingine zinazoziba au kuvamia njia za maji, zimeendelea kuwa vyanzo vingine vya kuongeza hatari ya mafuriko katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Chalamila alisema taka zinazotupwa katika maeneo yasiyofaa huziba njia za maji na kusababisha maji kushindwa kufuata mkondo wake wa kawaida.

Kwa sababu hiyo, mkoa unataka kampeni ya usafi iende sambamba na maandalizi ya El Niño.

Msimbazi kitovu cha mpango Moja ya maeneo yanayopewa uzito katika maandalizi hayo ni Bonde la Mto Msimbazi, ambalo kwa miaka mingi limekuwa miongoni mwa maeneo yenye historia ya mafuriko Dar es Salaam.

Chalamila amesema kazi ya kusafisha mito inapaswa kuendelea ili kupunguza mrundikano wa udongo, mchanga na taka na kuongeza uwezo wa maji kusafiri kwa haraka kuelekea baharini.

Serikali tayari inaendesha Mradi wa Maendeleo ya Bonde la Mto Msimbazi unaolenga, pamoja na mambo mengine, kuimarisha uwezo wa Dar es Salaam kukabiliana na mafuriko na kuboresha maendeleo ya maeneo yanayokumbwa na mafuriko.

Kwa mujibu wa Chalamila, kazi zinazohusiana na Mto Msimbazi zinajumuisha uboreshaji wa kingo na njia ya mto ili kuongeza uwezo wake wa kupitisha maji.

Mkoa pia unategemea miradi mingine ya mifereji na miundombinu ya kudhibiti maji katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Lengo, kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, ni kuunganisha njia ndogo za maji na mifereji mikubwa ambayo inaweza kuyapeleka maji kwenye mito na hatimaye baharini.

Somo la El-Niño ya 2023/24 Uzito wa maandalizi hayo unaonekana vizuri zaidi ukiangalia kilichotokea mara ya mwisho Tanzania ilipokumbwa na mvua kali zinazohusishwa na El Niño.

Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi ya CAG kuhusu usimamizi wa mafuriko nchini inaonyesha kuwa mafuriko yaliyohusishwa na mvua za El Niño kati ya Oktoba 2023 na Machi 2024 yalichangia ongezeko kubwa la vifo vilivyotokana na mafuriko na majanga yanayohusiana nayo.

Kwa mujibu wa taarifa za Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura zilizotumiwa na CAG, vifo vilivyohusishwa na mafuriko vilifikia 130 mwaka 2023/24, kutoka 64 mwaka 2020/21.

Miongoni mwa matukio makubwa zaidi lilikuwa janga la Hanang, Manyara, ambako mvua kubwa zilisababisha mafuriko na maporomoko ya udongo Desemba 2023. CAG inasema tukio hilo lilisababisha vifo 89.

Athari hazikuishia kwa maisha ya watu kwani CAG ilibaini kuwa eneo la mazao lililoathiriwa na mafuriko nchini liliongezeka kutoka hekta 1,795 mwaka 2020/21 hadi hekta 5,381 mwaka 2023/24.

Dar es Salaam yenyewe ilipata pigo kubwa katika miundombinu ambapo takribani kilomita 146.08 za mtandao wa barabara ziliharibiwa na mvua za El-Niño mwaka 2023.

Benki ya Dunia imekadiria kuwa majanga ya hivi karibuni yaliyohusisha mvua za El Niño na vimbunga yaliathiri zaidi ya watu 200,000 nchini na kusababisha uharibifu wa jumla wa takribani dola milioni 368.

Hiyo ndiyo historia ambayo Dar es Salaam haitaki ijirudie.

Udhaifu wa maandalizi waonwa Pamoja na mambo mengine, Ripoti ya CAG ina jambo jingine muhimu kwa maandalizi ya sasa.

Ukaguzi huo ulibaini kwamba licha ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutoa tahadhari za mapema kuhusu ujio wa mvua za El-Niño, maandalizi ya kukabiliana na athari zake hayakuwa Hilo linaweka kipimo muhimu kwa Dar es Salaam mwaka huu.

Mafanikio hayatapimwa kwa idadi ya tahadhari zinazotolewa kabla ya mvua, bali kwa kiwango ambacho tahadhari hizo zimesababisha hatua zinazoonekana - mifereji iliyosafishwa, mito iliyofunguliwa, maeneo hatarishi yaliyotambuliwa, wananchi waliopewa taarifa na mifumo ya uokoaji iliyoandaliwa.

Serikali tayari imetoa maelekezo 13 ya kitaifa ya maandalizi ya El-Niño. Mikoa na halmashauri zimeagizwa kutambua maeneo hatarishi mapema, kufanya tathmini za vihatarishi na kuwahamasisha wananchi walio katika maeneo hatari kuhamia sehemu salama.

Tatizo la taka lapewa uzito Chalamila anaunganisha moja kwa moja maandalizi ya El Niño na usafi wa jiji na kusema haiwezekani kuzungumzia kupunguza mafuriko wakati taka zinaendelea kutupwa kwenye mifereji, mito na maeneo mengine ambayo maji yanapaswa kupita.

Mkoa umeagiza kuanza kampeni maalumu ya usafi, huku halmashauri zikitakiwa kuongeza uwezo wa ukusanyaji wa taka na kuzuia utupaji holela.

Pia ametaka matumizi ya vifaa vya kisasa katika shughuli za usafi na ushirikishwaji mkubwa wa sekta binafsi katika ukusanyaji na uchakataji wa taka.

Wananchi waanza maandalizi Kwa upande mwingine, wananchi wameanza kuchukua tahadhari kuhusu uwepo wa mvua za el nino kwa kurekebisha mazingira yao pamoja na kununua vyakula kwa wingi.

Pambazuko imeshuhudia katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam wananchi wakizibua mitaro katika maeneo yanayowzunguka, wakifyeka na kuziba maeneo yenye hitilafu kama kuezeka upya mabati.

Katika maeneo ya masoko kama Kariakoo, Tandika, Stereo na mengine wafanyabiashara wengi wameongeza oda ya biashara zao ili kuwawezesha wateja wao kununua kwa wingi lakini pia kujiandaa na el nino.

Wakazi wa mkoa huo nao wameitika mwito wa serikali kuanza kuchukua hatua mapema za kujihadhari na ujio wa mvua hizo kubwa.

  • El-Niño
  • Dar es Salaam
  • Mafuriko
  • Maandalizi

Soma Pia