Habari
Siyo kampeni ya kusubiri wageni
Rais Samia Suluhu Hassan WIKI mbili baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuukosoa waziwazi uchafu katika Jiji la Dar es Salaam, mkuu wa mkoa huo, Albert Chalamila, amekiri kuwa mamlaka “zilijisahau” na sasa ametangaza mkakati mpya unaolenga kubadilisha mfumo wa kukusanya taka na tabia za wakazi.
Chalamila amesema dhamira kubwa siyo kufanya usafi kwa muda ili kujibu karipio la Rais Samia, bali kujenga utamaduni mpya utakaofanya usafi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya wakazi wa Dar es Salaam.
“Kwa wazi kabisa tumekubaliana, kuanzia ngazi ya mkoa, halmashauri hadi kwa wananchi, kwamba tulijisahau. Tulijisahau kwa muda,” alisema Chalamila katika mkutano na wahariri na viongozi wa jiji Septemba 17.
Kikomo cha bure kimefikia
Umesoma makala 3 za bure mwezi huu
Jiunge ili kuendelea kusoma bila kikomo, au ingia kama tayari una uanachama.
Mwezi
TSh 8,000
kwa mwezi
Mwaka
TSh 80,000
kwa mwaka
Au fungua akaunti ya bure ili hesabu yako ifuatane nawe kwenye vifaa vyote.
Lipa kwa M-Pesa · Mixx by Yas · Airtel Money · HaloPesa