Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Michezo

‘Debi’ ya kutoana roho kutikisa

BAADA ya kuanika silaha zao za kwenda nazo vitani msimu wa 2026/27, miamba ya soka la Tanzania; Simba na Yanga, zitapepetana katika mchezo wa Ngao ya Jamii, ukiwa ni ufunguzi wa pazia la msimu mpya wa mashindano ya ndani.

Jumatatu, 10 Agosti 2026 · 17:15Dakika 1 kusomaToleo 177, uk. 42

Mtanange huo utarindima ndani ya Dimba la New Amani Complex Zanzibar Jumanne Agosti 12, 2026, kati ya Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL), dhidi ya Simba, mabingwa wa Kombe la Shirikisho (CRDB FC).

Kinachokwenda kufanyika ni wachezaji wa timu zote kuonyesha kile roho inapenda ama ndo, utanitoa roho itaanza mapema kuchafua shuka la kumbato zito la matarajio ya msimu?

Simba ndio kinara wa mataji ya Ngao, ikiwa imechukua mara 10 kati ya 15 ilizocheza, huku Yanga wakichukua mara 9 kati ya mara 15 ambazo wamecheza.

Ukivitazama vikosi vya timu zote mbili vina mabadiliko ya wachezaji, lakini Yanga ndiyo ina maingizo mapya mengi ya wachezaji ambayo ni zaidi ya 10, wakiwemo nyota sita wa kimataifa wakiongozwa na Peter Shalulile aliyetokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Kwa upande wa Simba mpaka sasa wamekuwa na maingizo sita huku nyota watatu wakiwa ni wa kigeni wakiogozwa na Ibrahim Doumbia kutoa Mali na watatu wakiwa wazawa.

Kwa upande wa mabenchi ya ufundi, Simba wanaye Steve Barker ambaye amekuwa na timu kwa zaidi ya miezi sita na kucheza Debi tatu, akishinda moja na kutoka suluhu moja na sare moja.

Yanga wako na kocha mpya, Manqoba Mngqithi, aliyechukua mikoba ya kudumu ya Pedro Goncalves.

Kufuatia maingizo hayo, kinachosubiriwa ni jibu la nani kucheka baada ya vita yao pale Ungaju viziwani Zanzibar, na nani atawatoa roho mashabiki kuelekea msimu mpya wa mashindano? Jibu ni dakika 90 za jasho na damu kwa kila upande.

  • Simba
  • Yanga
  • Ngao ya Jamii

Soma Pia