Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Michezo

Matamasha yatia fora wakuu wa Dabi ya Dar

KILA mwenye macho ameona kile ambacho kimeonyeshwa na miamba ya Soka la Tanzania, Simba na Yanga, vikongwe kutoka Kariakoo Dar es Salaam kwenye tamasha lao la 18 la ‘Simba Day’, na ‘Mwananchi Day’ 2026, ambapo wamezitambulisha silaha zao za msimu mpya wa Mashindano wa 2026/27.

Jumatatu, 10 Agosti 2026 · 17:15Dakika 1 kusomaToleo 177, uk. 41

Walianza Simba katika kilele cha siku yao, ambayo kwao ni utambulisho wa kuanzishwa kwao, Agosti 8, 1936.

Jana ilikuwa ni sherehe za kusherehekea miaka 90 ya historia, vita, changamoto na ukomavu katika maisha ya soka kwa burudani za kila aina na utambulisho wa kikosi chao katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam juzi.

Ukiachilia nyota waliokuwepo msimu uliopita, nyota wapya wazawa ni Kelvin Nashon, Bakari Msimu na Nathaniel Chilambo, huku wageni ni Ibrahim Jabaar, Ibrahim Doumbia, Keletso Makgalwa na wote wameonysha nini wamekuja kukiongeza ndani ya Simba msimu ujao.

Moja ya burudani kubwa la tamasha la Jumamosi ilikuwa ni namna Meneja Habari na Mawasilaino wa Simba, Ahmed Ally alivyoingia katika Uwanja wa Uhuru akiwa na Simba wawili waliofungiwa kwenye kizimba jambo ambalo limeacha alama ya ubunifu katika burudani na ushereheshaji.

Walimalizia wananchi katika kilele cha wiki yao ya Mwananchi ambayo nayo inazidi kukita mizizi ya kuwakutanisha Wananchi wote kwa burudani, utambulisho na mwanzo wa pamoja wa msimu mpya.

Sherehe ya Yanga jana Jumapili ilikuwa na 'vibe' kubwa na uwanja kuchangamka mno kwa burudani lukuki kuliko ilivyokuwa kwa watani wao, Simba ambapo pia walifungwa na Timu ya Polisi Kenya kwa bao 1-0.

Jana Timu ya Wananchi ilionyesha wachezaji wake wapya na uwanja ulilipuka kwa furaha baada ya kutambulishwa Shalulile.

Wengine walioamsha kelele zaidi ni Farouk Komara, Fred Ngoma, Housseine Zakouani, Albert Kangwada, Ibrahima Toure, huku wazawa wakiwa ni Eric Mwijage, Mohamed Musa, Abdulnasir Muhamed, Hussein Mihambo, na Juma Abushiri.

Sasa kinachosubiriwa na wanachama, mashabiki na wapenzi wa soka ni kuona nini kinavunwa na kila timu na hatimaye kutwaa ubingwa wa ligi ya ndani au nje ya Tanzania.

  • Simba
  • Yanga
  • Soka

Soma Pia