Michezo
Mnyama anguruma, Wananchi si haba
WAWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) hatua za awali, Klabu ya Simba imeanza kampeni yao msimu wa 2026/27 kwa ushindi wa bao (0-1) dhidi ya Mighty Wanderers ugenini nchini Malawi.
Ushindi huo unaweka hai matumaini ya kusonga hatua za mtoano kuwania kutinga hatua ya makundi.
Mchezo huo ulipigwa Augosti 6, 2026 katika Dimba la Bingu, Uwanja wa Taifa la Malawi, na kushuhudia Simba, licha ya kupata matokeo GAZETI hili lilianzishwa 2021, kuandaliwa na kusambazwa na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (Tampa) na kusajiliwa na Serikali ya Tanzania, kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) na kupewa leseni namba - 00000448. Linaendeshwa kwa ushirikiano wa mzunguko – kwa kila nchi, wa mwaka mmoja na waandishi wa Tanzania, Kenya, Uganda, DRC na Rwanda.
mazuri, walipata mchezo mgumu katika muda wa dakika zote 90.
Bao la Simba liliwekwa kambani na Anicet Oura baada ya kutumia vyema makosa ya walinzi wa Mighty Wanderers kushindwa kudhibiti mpira ulipigwa na mlinda lango Jibrila Kasali.
Kwa ushindi huo Simba inarejea nchini Tanzania ikiwa na kazi moja tu ya kumalizia dakika 90 za mkondo wa pili kupata ushindi wa jumla na kusonga mbele.
Wakati huohuo, Timu ya Yanga ilipata sare ya bao (1-1) dhidi ya Gaborone United, mchezo uliopigwa nchini Botswana Augosti 05, 2026.
Iliwahitaji Yanga SC kusubiri bao la Selemani Mwalimu dakika za nyongeza kipindi cha pili kuweza kusawazisha na kupata sare hiyo ugenini baada ya kutanguliwa na wenyeji wao kipindi cha kwanza kwa mpira wa ikabu.
Sare hiyo imeweka hai matumaini kwa Wananchi kya kusonga mbele hatua ya mtoano ambapo katika dakika 90 zitakazopigwa jijini Dar es Salaam wikiendi hii, Yanga watahitaji kupata ushindi ama suluhu ili kusonga mbele.
NI wazi si matokeo yaliyotarajiwa na mashabiki wengi wa miamba hiyo ya Soka la Tanzania kutokana na aina ya wapinzani wao, lakini mchezo wa kandanda unachezwa hadharani na kila mmoja kushuhudia namna ambavyo kete huchangwa na pande zote mbili.
Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.
- Simba
- Yanga
- CAF Champions League