Habari Kuu
Democrats yashinda bunge, sasa kupunguza kasi ya uamuzi wa Rais Trump
Sasa kiburi cha Rais Trump katika uamuzi huenda kitapungua kwa kiasi kikubwa kwani atadhibitiwa na wabunge wa chama cha upinzani cha Democrats, ambao jana walishinda viti vingi.

CHAMA cha Democrats nchini Marekani kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa muhula uliofanyika jana, Novemba 3, 2026, na kunyakua udhibiti wa Bunge la Seneti kutoka kwa Republican, chama cha Rais Donald Trump.
Democrats pia wameshinda viti vya kutosha kudhibiti Baraza la Wawakilishi, hatua inayobadilisha mizania ya nguvu katika siasa za Marekani wakati Rais Trump akibakiza miaka miwili ya muhula wake.
Ushindi huo umejumuisha majimbo yaliyokuwa ngome za Republican, yakiwamo Texas, Kansas, South Carolina na Ohio, ambako wagombea wa Democrats wamewashinda wapinzani wao.
Matokeo hayo yanawapa Democrats nafasi ya kuimarisha usimamizi wa serikali, kuanzisha uchunguzi wa kibunge, kudhibiti matumizi ya fedha na kupinga baadhi ya uteuzi na sera za Trump.
Hata hivyo, mamlaka yao mapya yataanza rasmi Januari 2027, baada ya wabunge waliochaguliwa kuapishwa.
Akizungumzia ushindi huo, Barack Obama, Rais (zamani) wa Marekani, amesema wapigakura wametoa ujumbe kwamba wanataka siasa zinazowaunganisha wananchi, badala ya kuwagawa, pamoja na viongozi wenye majibu ya changamoto zinazowakabili.
Katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Obama amewapongeza wagombea wa Democratic na kuwataka kutumia ushindi huo kuleta mabadiliko, kuzuia madhara zaidi na kuweka msingi wa mustakabali wa Marekani.
Uchaguzi huo umeelezwa kuwa kipimo cha kupima uungwaji mkono wa Trump, huku gharama kubwa za maisha, vita vya Iran na wasiwasi kuhusu utawala wake vikichangia matokeo hayo.
Sasa Trump atalazimika kushirikiana na Bunge linalodhibitiwa na wapinzani wake ili kupitisha sehemu muhimu za ajenda yake.
Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.
- Marekani
- Uchaguzi
- Rais Trump
- Obama
- Democrats
- Republican