Burudani
Diamond ampagawisha Ayra Starr
NYOTA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz, ampagawisha msanii kutoka Nigeria, Ayra Starr katika tamasha lake la D Platinum All White Party V.V.I.P lililofanyika jijini Lusaka, Zambia juzi Ijumaa.
Ayra Starr ambaye alionekana akiimba neno kwa neno nyimbo za Diamond wakati wa tamasha hilo, huku akifurahishwa na ‘performance’ ya msanii huyo.
Diamond ambaye alikonga nyoyo za Wazambia hao kuanzia mapokezi yake katika Uwanja wa Ndege wa Lusaka, ambapo alipokelewa na mashabiki wengi wakiwa wamebeba zawadi za maua.
Pia Diamond Platnumz alitumbuiza kwenye tamasha lingine la African Concert juzi Jumamosi jijini Lusaka - Zambia.
DiamondDiamond ampagawishaampagawisha Ayra StarrAyra Starr Mwa FA: Mr Cheeks ameufurahia muziki wangu.
- Diamond Platnumz
- Ayra Starr
- Bongo Fleva
- Zambia