Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Burudani

Nandy amsaini Linah The African Princes

MSANII wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya The African Princess, Nandy, amemtambulisha rasmi msanii Linah kuungana naye.

Jumatatu, 7 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 181, uk. 36

Linah ametambulishwa katika lebo hiyo usiku wa kuamkia Septemba 4, 2026 katika ukumbi wa Mlimani City. Uzinduzi uliyoambatanisha na wimbo wa kwanza wa msanii huyo uliyopewa jina la ‘Raha.’ Akizungumza katika uzinduzi huo, Nandy amesema katika safari yake ya muziki amekuwa akimfuatilia Linah kama role model wake.

“Linah ana kipaji kikubwa, nilikuwa najiuliza kwanini hatoi nyimbo wakati ana kipaji kikubwa?

Nilikuwa namwuuliza lakini kuna siku akaja kunifungukia kwamba ana changamoto na amekata tamaa,”

amesema Nandy.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • Nandy
  • Linah
  • Bongo Fleva

Soma Pia