Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Uhusiano

Fanya yote, usimsahau Mungu

NI wiki nyingine tena tunakutana katika safu hii ya uhusiano ili kufahamishana mambo mbalimbali ya maisha.

Jumatatu, 24 Agosti 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 179, uk. 34
Fanya yote, usimsahau Mungu
Fanya yote, usimsahau Mungu — Picha kutoka Maktaba

Wiki iliyopita nilizungumza umuhimu wa wazazi kutenga muda wa kukaa na watoto wao na wiki hii nitazungumza namna ya kufanya mambo yako bila kumsahau Mungu kwa kumpatia shukrani na maombi.

Katika maisha ya kila siku tunakimbia shule, kazi, biashara na familia lakini wengi wetu tumekuwa tukimsahau Mungu na kuegemea kwenye maisha ya kidunia pekee bila kufahamu kuwa mafanikio yetu bila msingi wa kiroho ni kama nyumba iliyojengwa juu ya mchanga.

Ikiwa utatumikia Mungu na mali utakuwa umetimiza wajibu wa msingi katika maisha yaani kuonyesha bidii, nidhamu na uwajibikaji.

Mungu ametupa akili, nguvu na muda.

Kuyatumikia vizuri majukumu yetu bila kumsahau na katika huduma kwa wengine ni ibada pia.

Kutomsahau Mungu ni kumbusho la kushukuru na kuomba mwongozo kutoka Kwake.

Tunapopanga bajeti, kuchagua marafiki, au kufanya maamuzi makubwa na kumweka Mungu mbele hutupa hekima na amani. Sala, toba na matendo mema vinatufundisha unyenyekevu na huruma.

Kwa jamii zetu tunazoishi kwa ujumla, ujumbe huu unatufundisha usawa; shughulika na dunia lakini shika na mbingu. Wazazi wafundishe watoto bidii na maadili, viongozi watumikie kwa uadilifu. Vijana wafanye kazi na pia waweke muda wa ibada na kujifunza.

Tufanye yote kwa mikono yetu na mioyo yetu ikiwa kwa Mungu, tunajenga jamii yenye maendeleo, upendo na matumaini ya kweli.

Tukutane wiki ijayo Kwa maoni na ushauri: hellen2ngoromera@ gmail.com Au simu: 0715 88 67 49.

  • Uhusiano
  • Imani

Soma Pia