Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Uhusiano

Msamaha huponya zaidi

NI wiki nyingine tena tunakutana nawe msomaji wangu kupitia safu hii kwa lengo la kupeana elimu na maarifa kuhusu masuala ya uhusiano.

Jumatatu, 7 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 181, uk. 34

Wiki hii nitazungumza umuhimu wa msamaha.

Msamaha ni dawa ya moyo uliojeruhiwa.

Unapomsamehe mtu unapooza kidonda ambacho chuki na kinyongo vimeacha.

Watu wengi hubeba uchungu kwa miaka bila kujua kuwa mzigo huo unawaumiza zaidi wao wenyewe kuliko aliyekosea.

Msamaha unamfungua mtu kutoka gereza la hasira, unapunguza msongo wa mawazo, unaboresha usingizi na hata unaimarisha afya ya moyo. Mtu aliyejaa kinyongo huishi kwa hasira na huzuni, lakini yule aliyesamehe huishi kwa amani.

Katika uhusiano msamaha ni mafuta. Hata ndugu wanagombana, marafiki wakikosana, mwalimu na mwanafunzi wakikoseana, tiba pekee ni msamaha.

Bila msamaha uhusiano unakufa taratibu lakini ukiwepo, hata majeraha makubwa yanaweza kupona na upendo unarudi tena.

Kiroho msamaha una nguvu. Dini zote zinatufundisha kusamehe ili nasi tusamehewe.

Msamaha pia ni ishara ya ukomavu na ujasiri, siyo udhaifu na unahitaji moyo mkubwa kuachilia na kuchagua amani.

Katika jamii nyingi watu wengi hukoseana na kuwekeana vinyongo, hushindwa kuelewana, hushindwa kuzungumza n ahata kusaidiana na chochote hata mmoja wao anapotokewa na tendo la huzuni au furaha. Wanakosea!

Msamaha si tu kwa ajili ya yule aliyekosea.

Ni tiba kwako kwanza. Unapotoa msamaha unajiponya, unajikomboa, na unaruhusu furaha irudi moyoni mwako.

Tujifunze kusamehe ili kuruhusu amani kutawala mioyoni mwetu.

Tukutane wiki ijayo.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • Uhusiano
  • Msamaha

Soma Pia