Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Uhusiano

Ujasiri humjenga mtoto

BILA shaka u mzima msomaji wangu wa safu ya uhusiano. Wiki hii nitazungumza umuhimu wa mtoto kufundishwa ujasiri.

Jumatatu, 14 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 182, uk. 34

Ujasiri ni jambo muhimu ambalo mzazi au mlezi anapaswa kulipanda kwa mtoto tangu wakati wa utoto wake.

Mtoto jasiri anakuwa mtu anayeweza kukabiliana na changamoto za maisha bila kukata tamaa.

Ujasiri unampa mtoto uwezo wa kutatua matatizo yake mwenyewe badala ya kulia au kukimbia, lakini pia unampa uthubutu wa kujaribu tena hadi kufaulu.

Unamjengea pia tabia ya kutokata tamaa shuleni au mahali popote atakapokuwa, pia humpunguzia hofu na wasiwasi.

Watoto wengi huogopa kuuliza maswali, kuzungumza mbele ya watu, au kukataa mambo mabaya waliyofanyiwa au kufanya.

Mzazi anapomfundisha mtoto kuzungumza ukweli na kusema ‘hapana’ anampa ngao dhidi ya udanganyifu na vitisho.

Humjenga kuwa kiongozi bora wa kesho. Mtoto jasiri akiwa mahali popote hutetea UjasiriUjasiri humjengahumjenga mtotomtoto mwenzie kwa mambo watakayokabiliwa nayo na katika jamii anakuwa mtu wa kutoa suluhu, siyo kulalamika.

Hata viongozi wengi wakubwa tulionao sasa historia ya utoto wao huonyesha kwamba walianza kuwa na ujasiri.

Pamoja na mambo mengine hali hiyo humlinda mtoto. Watoto waoga ni rahisi kudanganywa au kuteswa kimya, lakini mtoto aliyefundishwa kufanya maamuzi pale anapofanyiwa jambo mfano kupiga kelele anapoteswa au kupatwa na kitu kisicho cha kawaida ili kujinusuru hawezi kutetereka.

Jamii inapaswa kuelewa kwamba kumfundisha mtoto ujasiri si kumfanya awe mkorofi bali kunamfanya awe na moyo wa uthubutu!

Mzazi au mlezi anayepanda mbegu ya ujasiri leo kwa mtoto wake anavuna mtu mzima asiyeogopa maisha kesho. Ujasiri ni kuchagua kufanya lililo sahihi hata moyo ukitetemeka.

Tukutane wiki ijayo, penye majaaliwa.

  • Uhusiano
  • Malezi
  • Watoto

Soma Pia